Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Abdalla Juma Saadala “ Mabodi” na
kushoto ni Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Nd. Abdulghafar
Idrissa akifanya kazi ya kukandika udongo katika nyumba ya mwananchi Bi.
Asha Abdalla wa Shehia ya Fuoni Migombani aliyebomokewa nyumba yake
kutokana na maafa ya mvua zilizonyesha juzi Unguja.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika harakati za ujenzi wa nyumba hiyo uko Fuoni Migombani Unguja.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika harakati za ujenzi wa nyumba hiyo uko Fuoni Migombani Unguja.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Abdalla Juma Saadala “ Mabodi” akitoa
shukrani zake kwa wananchi mbali mbali walioshiriki katika ujenzi huo na
kuhakikisha Bi.Asha Abdalla anapata makaazi ya kuishi. Picha na Afisi
Kuu CCM Zanzibar.
………………………………………………………
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
WANANCHI
visiwani vya Zanzibar wameshauriwa kuendeleza kwa vitendo Utamaduni
wa uzalendo wa kusaidiana wakati wa maafa mbali mbali yanayotokea
nchini bila kujadili tofauti za kisiasa na kidini.
Wito
huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma
Saadala “ Mabodi” mara baada ya ujenzi wa nyumba ya Balozi wa Nyumba
kumi Bi. Asha Abdalla Baruti iliyobomoka kutokana na maafa ya mvua
zinazonyesha nchini, huko Fuoni Migombani.
Dkt.
Mabodi alisema maafa yanapotokea hayachagui sehemu ya kuathiri bali
yanawakumba wananchi wote hivyo ni muhimu wanajamii kushirikiana kwa
mambo ya kijamii na kimaendeleo na kuacha siasa za utengano na chuki.
Ujenzi
huo umefanyika kutokana na agizo la Naibu Katibu Mkuu huyo alipowataka
uongozi wa CCM na UVCCM Wilaya ya Dimani Unguja, kumjengea makaazi ya
muda mwananchi huyo ambaye hakuwa na sehemu ya kuishi kutokana na
nyumba yake kuharibiwa na mvua zilizonyesha hivi karibuni.
Alisema
hatua ya Chama hicho kutoa msaada na kushiriki katika masuala ya
shughuli za kijamii kwa wananchi itakuwa ni utamaduni endelevu kwa
Unguja na Pemba.
Alieleza
kwamba lengo la CCM kutoa msaada wa kujenga makaazi ya dharura kwa
wananchi wakati wa kipindi hichi cha maafa ni kuendeleza kwa vitendo
siasa za waasisi wa vyama vya ASP na TANU ambao walishiriki katika
masuala mbali mbali ya kitaifa na kimataifa kwa lengo la kuwa karibu na
wananchi waliowapa ridhaa ya uongozi.
Pia
alisema wakati wa Kampeni za Uchaguzi CCM ilikuwa ikienda kwa wananchi
katika maeneo mbali mbali kuomba kura za kuiweka madarakani hivyo hata
kwa kipindi cha maafa na changamoto zinazoikabili jamii ni lazima kirudi
kwa wananchi kuwaunga mkono na kuwafariji kwa vitendo.
Naibu
Katibu Mkuu huyo alisema CCM ya sasa Viongozi wa ngazi mbali mbali ndani
ya Chama na Serikali kurudi kwa wananchi kujua changamoto
zinazowakabili na kuzifanyia kazi kwa wakati ni jambo la lazima na sio
la hiari.
“
Nasaha zangu kwa wananchi ni kwamba pindi yakitokea maafa hasa magfuriko
tusaidiane kwanza kupitia umoja wetu katika mitaa mbali mbali
tunayoishi kwa kuwahifadhi katika maeneo salama wenzetu wanaopata maafa
huku tukisubiri serikali zetu zichukue hatua za kutoa misaada.”, alisema
Dkt. Mabodi.
Pamoja
na hayo aliwataka vijana nchini kuwa mstari wa mbele kwa kujitokeza
muda wowote kusaidia masuala ya ujenzi wa miundombinu iliyoharibiwa na
maafa ili nchi iweze kujivunia uwepo wa kundi hilo ambalo ndio nguvu
kazi ya taifa.
Pia
aliwataka viongozi wa kisiasa nchini kuondokana na mazoea ya kulalamika
na kulaumu serikali hasa katika kipindi hichi cha maafa na badala yake
wawe sehemu ya kuwahamasisha wafuasi wao wajitolee kuwasaidia watu
waliofikwa na maafa huku serikali ikiendelea kutafuta ufumbuzi wa kudumu
wa kutatua tatizo hilo.
Naye
Mwakilishi wa Jimbo la Fuoni, Mh. Yussuf Hassan Iddi amesema jimbo hilo
litaendelea kusaidia awamu kwa awamu wananchi mbali mbali waliopata
maafa ili waweze kurudi katika hali yao ya kawaida.
Alisema
uongozi wa jimbo hilo baadae utahakikisha unajenga nyumba ya kudumu kwa
mwananchi huyo ili aweze kupata uhakika wa makaazi yake.
Kwa
upande wake Mbunge Mteule wa Bunge la Afrika Mashariki kwa tiketi ya CCM
, Dkt.Abdulla Hasnuu Makame alisifu hatua zilizochukuliwa na CCM kwa
kuendeleza utaratibu wa kuwafariji wananchi wakati wa matatizo mbali
mbali ya kitaifa .
Aliahidi
kuiwakilisha vyema CCM katika Bunge hilo ili fursa mbali mbali
zinazopatikana ziweze kusaidia katika kuimarisha miradi ya kijamii hasa
kuongeza miundombinu ya barabara, Elimu, Afya na ajira kwa vijana.
Mapema
Bi. Asha Abdalla ameishukru CCM na wananchi wote walioshiriki katika
zoezi la kumjengea nyumba yake na kuongeza kwamba hatua hiyo imemfariji
na kumpa nguvu za kuendelea kufanya kazi za kujipatia kipato kwa ufanisi
zaidi.
0 comments:
Chapisha Maoni