Baada
ya Rais John Magufuli hivi karibuni kutoa agizo kwa watumishi wa umma
9,932 waliobanika kuwa na vyeti vya kugushi, kuondoka kazini mara moja
na kwamba watakaobakia kazini hadi Mei 15 wakamatwe ili sheria ichukue
mkondo wake ikiwemo kufungwa jela miaka 7, na kuzitaka mamlaka
zilizowaajiri kukata mishahara yao.
Agizo
hilo limepelekea uhaba wa watumishi wa umma katika baadhi ya hospitali
ambapo Mkoani Iringa kwenye hospitali ya Manispaa hiyo ya Frelimo
imeondokewa na watumishi 10, wakati zahanati za Msisiwe na Ibumu
zilizopo wilayani Kilolo zikibakiwa na mtumishi mmoja mmoja.
Aidha,
Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Iringa Dkt. William Mafwere, amesema
kati ya watumishi 50 waliobainika kuwa na vyeti vya kugushi, 25
wanatoka idara ya afya huku akibainisha kwamba idara ya elimu mkoani
hapo haijaathirika na zoezi hilo.
Na Regina Mkonde