**
Ofisa wa Polisi ameuawa usiku wa kuamkia leo katika eneo la Kinyerezi Kanga wilayani Ilala.
Taarifa
zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni
zinasema aliuawa nyumbani kwake. Hata hivyo hakumtaja jina lake.
Taarifa
zaidi zimesema ofisa huyo wa Polisi alikuwa akifanya kazi wilaya ya
Kibaha na alikuwa amehamishiwa mkoa wa Kigoma hivi karibuni.
Kamanda Hamduni amesema taarifa zaidi kuhusu polisi huyo zitatolewa baadaye.
“Ni kweli kuna ofisa wa Polisi ameuawa niko eneo la tukio naomba mniache nifanye kazi tutawapa taarifa baadaye,” alisema.
0 comments:
Chapisha Maoni