

Katika taarifa iliyoripotiwa na BBC njiwa huyo alikamatwa baada ya
kushindwa kuruka baada ya kuzidiwa na uzito wa dawa hizo ambapo alikuwa
amebebeshwa kibegi kidogo mgongoni kilichojazwa vidonge 178 vya dawa
zinazoaminika kuwa na thamani kubwa akidaiwa kutoka Iraq.
Mbinu hii ya kutumia njiwa katika kusafirisha dawa za kulevya imekuwa
ikitumika sana kwenye sehemu zenye ulinzi mkali ambapo mwaka 2015
iliripotiwa kukamatwa kwa njiwa aliyebeba dawa za kulevya aina ya
Cocaine na Bangi katika ukuta wa jengo la gereza Costa Rica.
0 comments:
Chapisha Maoni