Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Viattel Tanzania (Halotel) Do Manh Hong,
amepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu
mashtaka saba likiwemo la uhujumu uchumi.
Mshtakiwa
Do Manh Hong amefikishwa mahakamani hapo na kuunganishwa na washtakiwa
wengine saba waliofikishwa mahakamani hapo mapema Mwaka huu.
Wote
kwa pamoja wanakabiliwa ma mashtaka kumi, kula njama. Kisimika mitambo
ya mawasiliano bila kibali cha TCRA, kutoa nyaraka za uongo, kusababisha
hasara kwa serikali ya Tanzania, ya milioni 459, kutumia mitambo ya
mawasilino ambayo haijathibitishwa na namba za simu.
Mbali
na Hong, washtakiwa wengine ni Dilshad Ahmed (36), Rohail Yaqoob(47),
Khalid Mahmood (59), Ashfaq Ahmad (38), Muhamad Aneess(48), Imtiaz Ammar
(33) wote raia wa Pakistan na Ramesh Kandasamy (36) raia wa Sri-Lanka.
Kabla
ya kusoma kwa mashtaka, wakili wa Serikali, Jehovanea Zacharias
aliiomba mahakama kumuunganisha mshtakiwa Hong na kuwasomea washtakiwa
wote makosa yao.
Imedaiwa
mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, kuwa mshtakiwa Ahmed,
Yaqoob, Mahamood, Ahmad, Anees, Kandasamy na Qammar Novemba 2016 Dar es
Salaam walikula njama ya kutumia vifaa vya mtandao.
Imedaiwa
kuwa, watuhumiwa walitengeneza mfumo wa kutumia huduma za mtandao kwa
lengo la kukwepa kodi ya kupokea na kusambaza simu za kimataifa bila
kibali cha TCRA.
Aidha
imedaiwa kuwa Novemba 20, 2016 waliingiza vifaa vya kielektroniki bila
ya kuwa na leseni na kuvisimika bila ya kuwa na kibali cha TCRA.
Imedaiwa,
washtakiwa waliunganisha vifaa hivyo na huduma za mitandao kwa lengo
la kupokea na kusambaza mawasiliano bila ya kuthibitishwa na TCRA.
Kwa
upande wa Kampuni ya Viettel Tanzania Limited na Do Hong wanadaiwa kati
ya Novemba 2016 na Februari 2017 maeneo ya ofisi za Halotel Victoria
Kinondoni walishindwa kuthibitisha taarifa iliyotolewa na Unex Company
Ltd kwa lengo la kusajili laini za simu 1000.
Kwa
upande wa washtakiwa Ahmed na wenzake sita wanadaiwa kuwa Januari 5
,2016 walitoa Cheti chakughushi cha usajili wa kodi chenye namba
100-864-210 kuonyesha imetolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania wakati si
kweli.
Mbali
na mashtala hayo, watuhumiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kuisababisha
hasara TCRA na serikali ya Tanzania kiasi cha milioni 459.
Hata
hivyo, washtakiwa wote hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani
hapo kwa kuwa mshtaka yanayowakabili yako nchini ya sheria ya uhujumu
uchumi.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 29,2017.