Na Dotto Mwaibale
MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka umebaki kuwa asilimia 6.4 kama ilivyokuwa mwezi uliopita.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Sensa
za watu na takwimu wa Ofis ya Taifa ya Takwimu,(NBS), Ephraim Kwesigabo,
alisema hii inamaanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na
huduma kwa mwaka ulioisha March 2017 imekuwa sawa na kasi ya upandaji
ilivyokuwa mwaka ulioisha.
Kwesigabo, alisema fahirisi za bei zimeongezeka hadi 109.4 mwezi April 2017 kutoka 1o2 mwezi April 2016.
"Mfumuko
wa bei kwa kipimo cha mwaka umebaki kuwa asilimia 6.4 kama ilivyokuwa
mwezi marchi 2017 kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka
ulioisha mwezi Aprili imekuwa sawa na mwezi Marchi 2017,"alisema
Pia
alisema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa
mwezi Aprili 2017 umeongezeka hadi 11.8 kutoka asilimia 11.0 ilivyokuwa
mwezi Marchi.
Aidha
mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwaka kwa bidhaa za vyakula nyumbani na
migahawani kwa mwezi Aprili 2017 umeongezeka hadi asilimia 12.0 kutoka
asilimia 11.7 mwezi Marchi 2017.
Alisema
badiliko la fahirisi za bei kwa bidhaa sisizo za vyakula umepungua
kidogo hadi asilimia 3.4 mwezi Aprili kutoka asilimia 3.6 mwezi Machi.
Akizungumzia
kuhusu ukuaji wa thamani ya shilingi, Kwesigabo alisema uwezo wa
shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia
shilingi 91 na senti 71, mwezi Aprili 2017 ikilinganisha na shilingi 92
na senti 21 ilivyokuwa mwezi Marchi 2017.