Mjomba wa mtoto ameeleza kuwa mtoto amekuwa akijiandaa asubuhi na mapema sana na anaaga anaenda shule lakini anapitia kwa huyo mzee na baadaye muda wa saa moja anaenda shule……
Mahusiano yameanza tangia January, mpaka sasa hivi ni mwezi wa nane na sisi mpaka tumekuja kugundua ni baada ya kutokea ugomvi, mke wake yule mzee amempiga na kumng’ata mtoto ameumia na sisi ndio tukajua hilo suala.
Mtoto wangu ana miaka kumi na nne na mzee huyo ana kama 60 mpaka 70 maana ni babu kabisa, sisi tulikuwa hatujui tulikuwa tunajua anaenda shule na alikuwa anamuaga bibi yake maana anakaa na bibi yake kwamba wanatakiwa kuwahi namba kumbe asubuhi anaanza kwanza kwa huyo baba.
Jumatano asubuhi walipokutana na huyo baba kupewa hela mara mke wa huyo baba akatokea akaanza kumshambulia na kumng’ata.