Mti wa ukwaju. Majani yake hutumika katika tiba ya kuongeza maziwa kwa mama anaye nyonyesha. |
1. Chukua majani ya mti wa Mvumbasi, unguza pamoja na majani ya mti wa mnungunungu, halafu changanya na mafuta ya taa lita moja. Matumizi: Utakuwa unatumia kujichua kwenye miguu kutwa mara tatu kwa muda wa siku thelathini. Utapata nafuu kubwa sana.
Tunda la topetope;Mizizi ya mtopetope hutumika katika tiba ya kuondoa uvimbe kwenye kizazi. |
2. TIBA YA KIKOHOZI: Tafuna majani ya mti wa mbaazi. Mbali na kutibu kikohozi, mti wa mbaazi, unatibu magonjwa mengine mengi. Mfano, mizizi ya mti wa mmbaazi, husaidia kutibu chango la kiume na kusafisha kibofu cha mkojo.
3. KUVIMBA KWA TEZI LA SHINGO: Kama una sumbuliwa na tatizo la tezi kuvimba, chukua unga wa Kamun Nyeusi, kisha changanya na sega la nyuki, halafu tumia kukanda kwenye tezi, kila siku kwa muda wa mwezi mmoja. Utapata mafanikio makubwa sana.
4. TIBA YA MAUMIVU YA MGONGO, MIGUU, NYONGA NA KIFUA KUPASUA:
Kama una sumbuliwa na maumivu ya mgongo, miguu, nyonga na kifua kupasuka, fuata maelekezo yafuatayo:
Chukua mafuta ya nyonyo robo lita, mafuta ya Kamun Nyeusi kiasi cha robo lita pamoja na mafuta ya karafuu robo lita , changanya pamoja halafu uwe unatumia kujichua sehemu yenye maumivu, kutwa mara tatu kwa siku thelathini. Utapata nafuu kubwa sana.
5. TIBA YA KWIKWI : Kama unasumbuliwa na kwikwi, fuata maelekezo yafuatayo : Chukua majani ya mwembe mkavu, pekecha kisha mpe mgonjwa atumie kuvuta kama sigara halafu awe anameza moshi. Tatizo la kwikwi litaisha.
6. Tatizo La Kukojoa Kitandani ; Kama una tatizo la kukojoa kitandani, tumia mizizi ya mbaazi kwa kuchemsha, na kunywa maji yake kutwa mara mbili kwa siku, kwa muda wa siku kumi na nne.
7. Tatizo la uvimbe kwenye kizazi : Kama una tatizo la uvimbe kwenye kizazi, chukua mizizi ya mtopetope, tumia kwa kuchemsha na kisha kunywa maji yake, mara tatu kutwa kwa siku thelathini.
8. Vidonda vya koo : Kama una tatizo la vidonda vya koo, chukua maji ya uvuguvugu kiasi cha nusu lita, kisha kamulia ndimu tatu fresh, halafu tumia kusukutulia. Utafanya hivyo mpaka, utakapo pata nafuu.
9. Malaria sugu : Kama una malaria sugu, chukua maji ya dafu moja, weka kwenye chombo kisafi, kisha kamulia ndimu saba, halafu tumia kunywa. Fanya hivyo mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni kwa siku tatu hadi saba. Hakika utapata matokeo mazuri sana.
10. Tiba ya tatizo la kutoa harufu mbaya kinywani, sehemu za siri, kikwapa na jasho lenye harufu mbaya : Chukua maji yaliyo lowekewa mchele kiasi cha lita moja, kisha tumia kunawia sehemu husika na kusukutulia mdomo. Utafanya hivyo mara tatu kwa siku hadi utakapo ridhika na matokeo unayo yahitaji.
11. Kwa wakina mama; Jinsi yakuzuia uchungu wamimba,maumivu yakiuno, maumivu wakati wahedhi, na damu itokayo bila mpangilio wasiku maalumu,Chukua majani ya mbigili yatwange halafu changanya navijiko vitatu vikubwa vya unga wa mti unaitwa msonobali kisha tumia kunywa glasi 1 yenye ujazo wa milimita mia mbili na hamsini, kutwa mara tatu hadi hali yako itakapokua nzuri
12. Tiba Ya Vidonda Vya Tumbo,Kisukari pamoja na Typhoid:
Chukua mizizi ya mti wa msongati pamoja na majani ya mkalatusi vitwange kwa pamoja kisha chemsha kwenye maji lita moja, halafu tumia kunywa glasi moja ya robo lita, mara tatu kwa siku kwa siku thelathini.
13. Tiba Ya Tatizo La Kukosa Hamu Ya Tendo La Ndoa Kwa Wanawake : Kama wewe ni mwanamke unaye sumbuliwa na tatizo la kukosa hamu ya tendo la ndoa, unaweza kutibu tatizo lako kwa kutumia vyakula mbalimbali kama ifuatavyo :
i. JUISI YA MIWA : Tumia kunywa nusu lita hadi lita moja ya juisi ya miwa, mara tatu kwa siku asubuhi, mchana na jioni kwa siku thelathini. Utapata matokeo mazuri. Mbali na kuwasaidia akina mama wenye tatizo la kukosa hamu ya tendo la ndoa, juisi ya miwa ina faida nyingine nyingi kitabibu. Moja kati ya faida kubwa za juisi ya miwa, ni uwezo wake mkubwa wa kusafisha figo. Hivyo hata wanaume wanashauriwa kutumia juisi ya miwa au miwa kwa wingi,kwa sababu inasaidia kusafisha figo, na figo ni moja kati ya ogani muhimu sana katika mfumo wa nguvu za kiume.
ii. MBEGU ZA FENESI : Chukua mbegu za fenesi kiasi cha robo kilo, kisha chemsha na maji lita mbili, halafu tumia kula pamoja na supu yake. Utafanya hivyo mara tatu kwa siku kwa muda wa siku thelathini. Hakika utapata matokeo mazuri sana. Unaweza pia kuzisaga na kutumia unga wake, kwa kuchemsha na kunywa, kwa kufuata utaratibu huo hapo juu.
iii. KOROSHO : Tumia kula korosho pakti moja yenye ujazo wa robo kilo, mara tatu kwa siku, asubuhi, mchana na jioni kwa siku thelathini. Yaani asubuhi, tumia robo kilo, mchana robo kilo na jioni robo kilo kwa siku thelathini. Utapata matokeo mazuri.
iv. MIHOGO MIBICHI : Tumia kutafuna walau vipande vitatu vya mihogo mibichi kwa siku, kwa muda wa siku thelathini. Yaani asubuhi utumie kipande kimoja kikubwa,mchana kipande kimoja kikubwa na usiku, utumie kipande kimoja kikubwa.
14. TIBA ASILIA YA TATIZO KIFUA KISICHO PONA KWA WATOTO WADOGO WALIO KUNYWA UCHAFU WAKATI WA KUZALIWA, PUMU, KIFUA KISICHO PONA KWA WATU WAZIMA,KICHOMI,KUWASHWA MWILI NAKUPALIWA WAKATI UMELALA USINGIZINI
Tiba Yake, chukua majani ya mpera kiasi cha kama viganja vinne, yaponde pamoja na magome ya muembe kiasi cha viganja vinne, na tunda la koma manga, twanga vyote kwa pamoja ( Yani majani ya mpera, magome ya muembe na tunda moja la komamanga ).
Ukisha maliza kutwanga, changanya na maji lita mbili halafu chemsha pamoja na lita moja ya asali mbichi ya nyuki wadogo.
Chemsha hadi itokote, halafu ipua dawa yako.
Matumizi : Kwa mtoto mdogo mwenye umri wa kati ya mwaka mmoja na miaka mitano, tumia kumpa kijiko kimoja kikubwa mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni n kwa siku saba.
Na kwa mtu mzima, tumia kunywa vijiko vikubwa viwili mara mbili kwa siku asubuhi na jioni, kwa siku ishirini na moja
15. KUJITIBU TATIZO LA MTOTO WA JICHO : Kujitibu mtoto wa jicho, tumia kunyunyizia jichoni matone mawili ya utomvu wa toto la ndizi. Fanya hivyo mara tatu kwa siku, asubuhi, mchana na jioni kwa siku thelathini. Utapata matokeo mazuri.
Mbali na kutibu tatizo la mtoto wa jicho, toto la ndizi, likichanganywa kitaalamu na wine ya mnazi ( Palm wine ) au mnazi, husaidia kutibu tatizo la kidole tumbo au appendix.
16. TIBA ASILIA YA KUPUNGUZA GESITUMBONI
Kuondoa gesi tumboni, kwa kutumia tiba asilia, chukua juisi ya kitunguu maji kiasi cha glasi moja yenye ujazo wa milimita mia mbili na hamsini,kisha changanya na asali mbichi kijiko kimoja koroga halafu tumia kunywa .
Utafanya hivyo mara tatu kwa siku kwa muda wa siku kumi na nne.
AU chukua kipande kimoja cha tangawizi,kiponde ponde kisha chemsha kwenye nusu lita ya maji pamoja na kijiko kimoja kikubwa cha asali mbichi ya nyuki wadogo, halafu tumia kunywa kutwa mara mbili kwa siku ishirini na moja.
AU ; Chukua asali mbichi ya nyuki wadogo kiasi cha robo lita, changanya na vijiko vitatu vikubwa vya unga wa Kamun nyeusi,kisha chemsha pamoja kwenye maji lita moja.Halafu tumia kula vijiko vikubwa vitatu kutwa mara tatu kwa siku ishirini na moja.
17. TIBA YA PUMU : Chukua magadi vijiko vikubwa vitatu, saga upate unga wake, kisha changanya na samli ya n’gombe vijiko 21 vikubwa na asali vijiko 30 vikubwa. Matumizi : Tumia kula vijiko vikubwa vitatu asubuhi, vitatu jioni na vitatu usiku kwa muda wa siku thelathini. Utapata nafuu kubwa sana.
18. TIBA ASILIA YA KIHARUSI NA KIFAFA:
Chukua mizizi mitatu ya mti wa ukwaju, mizizi mitatu ya mti wa mkungu, mizizi mitatu ya mpapai, pamoja na mizizi mitatu ya mti wa ufwambo. Iponde ponde yote kisha chemsha kwa pamoja kwenye maji ya lita tatu hadi yachemke. Tumia kumpa mgonjwa glasi moja, kutwa mara tatu kwa siku thelathini. Mgonjwa wako atapata nafuu kubwa sana.
19. TIBA ASILIA YA FANGASI ZA KWENYE DAMU, UKURUTU, UPELE, MCHAFUKO WA DAMU, PAMOJA NA KUWASHWA KWAMWILI.
Chemsha robo kilo ya majani ya mti wa mdimu kwenye maji kiasi cha lita mbili. Maji yakisha tokota, ipua chuja, halafu tumia kunywa glasi mbili asubuhi, mbili mchana, mbili jioni. Utafanya hivyo kwa muda wa siku thelathini. Hakika utapata nafuu kubwa sana.
20. TIBA ASILIA YA MARADHI YA FANGASI ZA MIGUU NA KUNUKA MIGUU.
Twanga majani ya mwarobaini robo kilo, chemsha na maji lita tano, kisha weka kwenye beseni halafu loweka miguu yako ndani ya beseni kwa muda wa lisaa limoja. Utafanya hivyo kutwa mara mbili kwa muda siku kumi na nne. Utapata matokeo mazuri sana.
AU chukua majivu kiasi cha robo kilo,changanya na robo lita ya juisi ya ndimu, kisha nyunyizia kwenye miguu, na ukae kwa lisaa limoja. Utafanya hivyo mara mbili kwa siku kwa siku thelathini. Japo inauma lakini ni tiba nzuri sana.
21. KUONGEZA MAZIWA KWA MAMA ANAE NYONYESHA : Chukua majani ya mti wa ukwaju, kiasi cha nusu kilo, kisha chemsha na maji lita tano. Tumia kunywa glasi tatu asubuhi, tatu mchana, tatu jioni kwa muda wa siku saba. Hakika utapata matokeo mazuri sana. Utakuwa unafanya hivyo kila mara utakapo hitaji kuongeza maziwa.