Jana usiku nilikwazika kufuatia matokeo
ya uchaguzi wa wawakilishi wa Tanzania kwenye Bunge la Afrika Mashariki (
EALA ). Kufuatia hasira hiyo nikaandika kuwa wakati mwengine unajiuliza
Kama unastahili kuwa kwenye nchi ambayo umo Kama raia.
Haikuwa sahihi Kabisa Kwa Kiongozi wa
ngazi yangu kujutia uraia wangu kwa sababu tu ya kundi la watu wachache
kuamua kuchagua wawakilishi wetu kwenye taasisi za kimataifa bila kujali
uwezo, uzoefu na weledi wa wawakilishi husika.
Ninajua hatua ya Sasa ya Mtangamano wa
Afrika Mashariki Ni hatua muhimu mno kwani Ni hatua ya kuelekea Umoja wa
Fedha ( Monetary Union). Ndio maana Mataifa mengine yamepeleka raia wao
mahiri Kabisa. Rwanda wamepeleka Waziri Mkuu mstaafu na Mawaziri 2.
Burundi imepeleka Waziri wake Wa Afrika Mashariki. Uganda imepeleka
Mawaziri Wastaafu. Kenya imepeleka Wabunge wazoefu na Wafanyabiashara
wakubwa. Hata mwanachama mpya Sudani ya Kusini imepeleka Waziri wa
zamani, Spika wa Bunge wa zamani na Jenerali wa Jeshi.
Hasira za kuipenda nchi yangu Ndio zilinipelekea kuandika nilivyoandika.
Naomba radhi kwa andiko lile na
ninalifuta. Hata hivyo, Wabunge wote wa vyama vyote wajue kuwa wameionea
Nchi yetu. Wameweka maslahi ya vyama vyao na mahusiano yao mbele ya
maslahi ya nchi yetu. Tanzania imepeleka 'amateurs' huko EALA. Huu ndio
ukweli mchungu na lazima usemwe. Itabidi kuwa na program maalumu ya
kuwafundisha wawakilishi wetu hawa. Kina Adam Kimbisa lazima wachukue
jukumu hili bila kujali usumbufu wake.
Anyways! My country, Right or Wrong.
Zitto Kabwe (MB)