Mchango
wa Mbunge wa Kuteuliwa(CCM), Salma Kikwete kuhusu kupinga wanafunzi
wanaopata mimba wakiwa shuleni kuruhusiwa kuendelea na masomo jana
ulizua gumzo bungeni kutokana na wabunge kugawanywa na suala hilo.
Hali
hiyo ilijitokeza wakati wabunge waliokuwa wakichangia hotuba ya bajeti
ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa Fedha 2017/18
bungeni jana.
Salma
amesema anapinga suala la watoto wanaopata ujauzito shuleni kuendelea
na masomo kutokana na mila, desturi, dini na mazingira.
Ameitaka Serikali kutafuta njia nyingine ya watoto hao kupata elimu badala ya kuwaruhusu kuendelea na masomo.
Akitoa
taarifa yake kwa mchangiaji Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally
Keissy alitaka mbunge yeyote ndani ya Bunge ambaye alianza kushiriki
mapenzi akiwa shuleni atoe ushuhuda bungeni kama aliweza kuendelea
vizuri kimasomo.
Amesema anaunga mkono wanafunzi wanaopata mimba wakiwa shuleni wasiruhusiwe kuendelea na masomo
0 comments:
Chapisha Maoni