Mkurugenzi
wa Michezo Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Yusufu Singo
(kulia) akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa mashindano ya mbio
ya Km 21 ya Dasani Marathon 2017 baada ya kuwakabidhi zawadi zao eneo
la Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay Dar es Salaam leo. Mshindi wa
kwanza, Augustine Sule (aliyesimama juu), Mshindi wa pili Stephano Huche
(wa pili kushoto) na mshindi wa tatu Said Makula. Kushoto ni Nalaka
Hettierachchi Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Coca Cola Kwanza
iliyodhamini mashindano hayo kupitia kinywaji cha maji ya Dasani.
Na Richard Mwaikenda
WAZIRI
wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe
ameyafagilia mashindano ya mbio ya Dasani Marathon 2017 yaliyofanyika
leo jijini Dar es Salaam.
Kauli
hiyo imetolewa kupitia kwenye hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na
Mkurugenzi wa Michezo wa wizara hiyo, Yusufu Singo wakati wa kukabidhi
zawadi kwa washindi wa mashindano hayo yenye umbali wa Km 10 na 21.
Pia
aliipongeza Klabu ya Dar Running Club kwa maandalizi mazuri
yaliyofanikisha mashindano hayo yanayodhaminiwa na Kampuni ya Coca Cola
Kwanza kupitia maji ya Dasani. Kampuni hiyo imeingia mkataba wa
kuyadhamini mashindano hayo kwa miaka mitano.
"Nawapongeza
nyote kwa kuchukua jukumu kubwa la kufanikisha maandalizi ya mbio hizi
ambayo siyo tu ni nzito bali muhimu katika mchakato mzima wa kujenga
utamaduni wa kuzijali afya zetu na ustawi wa familia zetu, uelewano
uliothabiti katika kutekeleza majukumu yetu ya kifamilia na kitaifa".
Alisema Mwakyembe.
Awali
akizungumza Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Coca Cola Kwanza, Nalaka
Hettierachchi alisema wanataka mashindano hayo yawe makubwa ambapo hivi
sasa wana mipango ya kuyapeleka pia katika mikoa mingine nchini.
Mashindano
hayo yaliyoshirikisha zaidi ya watu 1000 kutoka maeneo mbalimbali
nchini, yalianzia na kuishia Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay na
kupita barabara mbalimbali za Jiji la Dar es Salaam ikiwemo ya Ali
Hassan Mwinyi.Aliyeibuka
kidedea katika mbio za wanaume za umbali wa Km 21 ni Augustine Sule,
wa pili akiwa Stephano Huche na Said Makula aliyeshika nafasi ya tatu.
Kwa
upande wa Wanawake aliyeibuka mshindi ni Jacquline Sakilu, wa pili
akiwa Noela Remmy na nafasi ya tatu ilikwenda kwa Antery John.Kwa
mbio za umbali wa Km 10, mshindi kwa upande wa wanaume alikuwa
Sylvester Seleman, wa pili akiwa Daniel Sinda na Paul Pascal alishika
nafasi ya tatu.Mshindi wa kwanza kwa wanawake alikuwa May Naari, wa pili
akiwa Sara Hitis na Asia Seleman aliyetwaa nafasi ya tatu.
Kwa upande wa walemavu aliyeshinda ni Shukuru Khalfan, wa pili alikuwa Mathias John na Jonis Stephano alishika nafasi ya tatu.Mshindi
wa kwanza wa mbio za Km 21 kwa upande wa wanaume na wanawake kila mmoja
alikabidhiwa sh. mil 1, wa pili sh. 750,000 na wa tatu sh. 600,000.
Baadhi ya washiriki wakimalizia mbio zao katika Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay
Washiriki wakivishwa medali baada ya kumaliza kukimbia katika mashindano hayo
Elizabeth wa NMB Bank akivishwa medali baada ya kumaliza mbio hizo
ni mbio kwa kwenda mbele
Mshiriki akiangalia muda alioutumia kukimbia. Kushoto ni Mwanariadha nguli wa zamani Juma Ikangaa
Juma Ikangaa akiwavisha medali washiriki wa mbio hizo
Mtoto akiwa miongoni mwa wakimbiaji
Wakimalizia kukimbia
Timu ya NMB Bank iliyoshiriki katika mashindano hayo
Wakifurahia kumaliza mbio
Wakiendelea na mazoezi baada ya mashindano
Juma Ikangaa akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa mbio za wanawake umbali wa Km 10, Mary Naali
Mshindi wa kwanza wa mbio za Km 10 wanaume, Sylvester Simon akikabidhiwa zawadi na Juma Ikangaa
Dorothy Kipeja wa Dar Running Club waandaji wa mashindano hayo, akimkabidhi zawadi mmoja wa washindi wa Km 21
Mshindi
wa kwanza wa mbio za umbali wa Km 21, Augustine Sule akipongezwa na
Juma Ikangaa alipokabidhiwa zawadi na Mkurugenzi wa Michezo, Yusufu
Singo (wa pili kulia)
Mshindi
wa kwanza kwa upande wa walemavu Shukuru Khalfan (katikati) akiwa na
Mkurugenzi wa Michezo, Yusufu Singo pamoja na Mkurugenzi wa Masoko na
Mauzo wa Coca Cola Kwanza, Nalaka.
Nahodha
wa timu ya riadha ya Radio EFM, Maulidi Kitenge akiwapongeza waandaji
wa mashindano hayo baada ya timu hiyo kushiriki ipasavyo.
Mtoto aliyeshiriki na kumaliza vizuri mbio hizo, akizawadiwa soda.
0 comments:
Chapisha Maoni