Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetangaza rasmi kumuunga mkono
Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa Kenya utakaofanyika mwezi Agosti
mwaka huu.
Msimamo
huo umetolewa jana katika mkutano wa Baraza Kuu la Chama hicho
unaofanyaki mjini Dodoma, ikiwa ni maamuzi ya Baraza hilo, na kutangazwa
rasmi na mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe.
Akizungumzia
uamuzi huo, Mbowe alisema sababu kuu ya uamuzi huo ni kugeukwa na
mgombea wa muungano wa ODM Raila Odinga, ambaye chama hicho kilikuwa
kikimuunga mkono mara zote.
Mbowe amesema "Kwa
muda mrefu chama chetu kimekuwa kikimuunga mkono Raila Odinga achukue
nafasi ya kuliongoza Taifa la Kenya. Mwaka 2015 ilipofika zamu yetu
rafiki yetu Raila Odinga alitugeuka na kumuunga mkono adui yetu. Sisi
kama Chama, safari hii tunamuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta na Umoja wa
vyama vinavyounda JUBILEE".
0 comments:
Chapisha Maoni