Na Tiganya Vincent, Tabora
Mkulima
mmoja Kitangili mkoani Shinyanga Francis Martin Kilalo (31)
anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora kufuatia kukutwa na sare
na vifaa vingine vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambavyo
anatuhumiwa kuvitumia kupateli nakuwadanganya kwa kuchukua fedha kutoka
kwa vijana wanaotafuta nafasi yakujiunga na Jeshi hilo.
Taarifa
hiyo imetolewa na Kamanda wa Mkoa wa Tabora, Wilbroad Mtafungwa
alipokuwa anaongea na waandishi wa habari ofisi kwake juu ya hatua
mbalimbali walizochukua katika kupambana na uhalifu mkoani humo.
Alisema
kuwa Polisi walifanikiwakumukamata mtuhumiwa huyo katika Hoteli ya JM
iliyopo Wilayani Igunga akiwa na sare mbalimbali za Jeshi la Wananchi
Tanzania (JWTZ) zikiwa na cheo cha Koplo ambavyo ni pamoja na kofia
tatu, begi, sweta, buti jozi moja, magwanda na mikanda mitatu.
Mali
nyingine zilikamatwa kwa mtuhumiwa huyo ni pamoja na fomu za likizo,
fomu za kujaza vijana wanaotaka kujiunga na Jeshi hilo na Jeshi la
Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa Sheria na hiari na mihuli zenye nembo
inayofanana na Jeshi hilo.
Kamanda
Mtafungwa alisema kuwa mtuhumiwa alikuwa akitumia nyaraka na sare za
Jeshi hilo kuchukua fedha kwa kuwadanganya na kuwatapeli wananchi
mbalimbali kwa kudai atawatafutia ajira katika majeshi ya Kujenga Taifa
na la Wananchi.
Kamanda
huyo wa Mkoa wa Tabora aliongeza kuwa mtuhimiwa huyo pia alikutwa na
barua kutoka Serikali za mitaa za Dar es salaam na gari aina ya Toyota
Starlet yenye namba za Usajili T633 ARF ambalo wanaendelea kuchunguza
uhalali wa umiliki wake na ambalo mtuhumiwa alikuwa akilitumia na
kuwafanya baadhi ya wananchi wamuamini kuwa atawasaidia kupata nafasi
katika majeshi.
Aliongeza
kuwa mtuhimiwa huyo na barua za maombi ya watu yakuomba kujiunga na
Jeshi, Fomu za Matibabu za Hospitali ya Jeshi ya Lugalo na kalaya Vyeti
vya kumaliza elimu ya Sekondari vya baadhi ya watu.
Kufuatia
tukio hilo alitoa witokwa waananchi waliowahi kutapeli ndani na nje ya
Mkoa wa Tabora kujitokeza katika vituo vya Polisi ili waweze kutoa
ushahidi utakasaidia kuonyesha ni jinsi gani walivyumizwa na mtuhumiwa
huyo .
Kamanda
Mtafungwa alisema kuwa Polisi inaendelea kushirikiana na JWTZ ili iweze
kubaini sare na vifaa hivyo alivipata wapi , kwa lengo lipi na ni nani
aliyompatia ili wahusika wote waweze kufikishwa katika vyombo vya Sheria
kwa hatua zaidi.
Aidha,
Kamanda huyo aliwaasa wananchi kuwa makini na matapeli wanaowadai fedha
na kuwadanganya kuwa watawatafutia kazi katika Majeshi kwani vyombo
hivyo vinaotaratibu wake ambao ndio unaotumika kuwapata vijana
wanaojiunga kwa mujibu wa sheria na wale wahiari na sio kwa kuchangishwa
fedha.
Wakati
huo huo Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora limefanikiwa kukamata watuhimiwa
17 kwa kukutwa na lita 205.25 za gongo wakati wa msako wa kukamata wa
watumiaji na wauzaji wa bidhaa hizo haramu.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Tabora Mtafungwa alisema kuwa watuhimiwa
watafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zao wakati wowote. Aidha, alisema
kuwa katika zoezi hilo pia Polisi ilifanikiwa kuteketeza ekari tano na
nusu za mashamba ya zikiwana uzito wa kilogramu 220 yalikuwa yamelimwa
katika Msitu wa Hifadhi wa Igombe wilayani Uyui.
Alisema
kuwa jitihada za kuwasaka watuhumiwa wa mashamba hayo zinaendelea na
kuwaomba wananchi wenye taarifa yawalipo wahusika walisaidie Jeshi la
Polisi ili wahusika waweze kufikishwa Mahakama kujibu tuhuma zao.
0 comments:
Chapisha Maoni