test

Jumamosi, 3 Juni 2017

Serikali kusafirisha mwili Mzee aliyechora Nembo ya Taifa Francis Maige Kanyasu


Mwili wa Mzee Francis Maige Kanyasu alimaarufu kwa jina la Mzee Ngosha ambaye anayetajwa kuwa ni moja wa wachoraji wa nembo ya Taifa aliyefariki tarehe 30 mwezi wa 5 unatarajiwa kusafirishwa leo  kuelekea Misungwi Mwanza.

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya (Maendeleo ya Jamii) imesema kuwa ndugu wa Mzee Kanyasu wamepatikana na sasa serikali itagharamia kusafirisha mwili wa mzee huyo mpaka Mwanza ambapo atakwenda kuzikwa huko.

Mwili wa Mzee Francis Maige unatarajiwa kuagwa leo  Jumamosi saa 2 asubuhi Hospitali Taifa ya Muhimbili kabla ya kuanza safari ya kuelekea Mwanza.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni