Mchungaji
wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima amefunguka na kusema
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad ni
rafiki yake hivyo alitaka kuonana naye ili aweze kujua Professa Ibrahim
Lipumba anaharibu vipi chama
Mchungaji
Gwajima amesema hayo jana alipokutana na waandishi wa habari baada ya
kumaliza mazungumzo na Katibu Mkuu huyo wa CUF na kusema aliamua
kukutana na rafiki yake huyo ili ajue hilo baada ya hapo yeye atajua
anafanyaje.
"Mimi
huyu ni rafiki yangu kwa hiyo nilitaka kujua Professa Lipumba anafanya
nini kuvuruga CUF, hivyo nilitaka kujua Lipumba amepatwa na nini mpaka
amevuruga chama chako na kiukweli mimi nilikuwa siufahamu vizuri huu
mgogoro ila saizi Seif ameniambia kwa hiyo na mimi nataka nitafakari
alichoniambia rafiki yangu ni ‘digest’ baada ya hapo nitajua nafanya
nini” alisema Gwajima
Kwa
upande wake Maalim Seif Sharif Hamad alisema kuwa amekaa na askofu
Gwajima na kuzungumza naye kwa kina juu ya mgogoro huo na kila mmoja
amemueleza mwenzake kile anachokifahamu na kusema ameamuchia askofu ili
na yeye atafakari juu ya jambo hilo baada ya hapo anaamini huenda askofu
akafanya jambo.
“Nimekaa
na askofu na kila mmoja akamweleza mwenzake yale ambayo anayajua, kwa
hiyo nimemweleza saizi kiundani kwa hiyo yeye ana ‘digest’ halafu askofu
yeye ataamua juu ya kile tulichuzungumza” alisema Maalim Seif Sharif Hamad