Aliyekuwa
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu amefariki dunia leo saa nne
asubuhi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)
Mdogo
wa marehemu, Shaibu Mwambungu amesema kaka yake alifariki dunia leo
asubuhi baada ya hali yake kubadilika ghafla akiwa hospitalini hapo.
Shaib
amesema taratibu za mazishi zitatolewa baadaye ambapo kwa sasa
anajiandaa kusafiri kutoka Songea kuja jijini Dar es salam kwa ajili ya
mazishi.