Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imesema kwamba huduma ya kupandikiza vifaa vya usikivu kwa watoto wenye matatizo ya masikio na watu wengine itaanza kutolewa Juni, mwaka huu.Huduma ya upandikizaji huo utaipunguzia serikali gharama za kuwapeleka wagonjwa wenye matatizo hayo nchini India
Kauli
hiyo imetolewa leo na Daktari Bingwa wa Masikio, Pua na Koo katika
Hospitali ya Muhimbili, Edwan Liyombo wakati wa kutoa elimu kwa wazazi
wa watoto wenye matatizo ya masikio jinsi ya kutunza vifaa vya usikivu
kwa watoto waliopatiwa huduma hiyo.
Dk
Liyombo amesema kwamba huduma itaanza kutolewa nwezi Juni, mwaka huu na
kwamba Hospitali ya Muhimbili imeboresha miundombinu na tayari imenunua
vifaa kwa ajili ya kuanza kwa huduma hiyo.
Kuhusu
gharama za mtoto mmoja kuwekewa kifaa cha usikivu amesema ni ndogo
kuliko akiachwa bila kupatiwa huduma hiyo kwani maisha yake yote atakuwa
hasikii wala hataweza kupata uelewa wa masomo shuleni.
“Sisi
tunaona hakuna gharama ya mtoto kuwekewa kifaa cha usikivu kwa sababu
huduma hii ataitumia katika maisha yake yote na akipelekwa shule atakuwa
na uwezo wa kusikia na kuzungumza, kwa kifupi atakuwa sawa kama watoto
wengine ambao hawana matatizo ya kusikia,” amesema Dk Liyombo.
Akizungumzia
lengo la kuwaita wazazi wa watoto wenye matatizo ya kutokusikia, Dk
Liyombo amesema ni kuwaelekeza jinsi ya kutunza vifaa hivyo na endapo
vina matatizo wanapaswa kutoa taarifa ili virekebishwe.
Amewataka
wazazi wenye watoto wenye matatizo ya kusikia kuwapeleka katika
hospitali hiyo kwa ajili ya kupatiwa huduma na pia amewataka kinamama
wajawazito kuudhuria kliniki ili kuchunguzwa afya zao pamoja na mtoto
kwa lengo la kuzuia mtoto kuzaliwa na tatizo la usikivu.
Daktari
Bingwa wa Masikio, Pua na Koo, wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH),
Edwin Liyombo akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu huduma ya
upandikizaji wa vifaa vya usikivu kwa watoto wenye matatizo ya masikio.
Kutoka kushoto ni Maneja wa Bidhaa, Shalini Srivatsan wa Kampuni ya
Vanguard (T) Limited na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Nitesh Patel.
Baadhi
ya wazazi wenye watoto ambao wana matatizo ya usikivu wakimsikiliza Dk.
Liyombo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo katika Hospitali
ya Taifa Muhimbili (MNH).
Maneja
wa Bidhaa, Shalini Srivatsan wa Kampuni ya Vanguard (T) Limited
akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu namna wanavyosaidia jamii
Watoto wenye matatizo ya usikivu wakiwa kwenye mkutano huo leo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa Hospitali ya
Muhimbili, Aminiel Aligaesha (kulia), Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanguard
(T) Limited, Nitesh Patel na Maneja wa Bidhaa wa kampuni hiyo, Shalini
Srivatsan (kushoto) wakimsikiliza Dk Liyombo wa Muhimbili kabla ya
kuanza kwa mkutano na waandishi wa habari wakiwamo wazazi wa watoto
wenye matatizo ya usikivu. Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH).