Mbunge
wa Kilombero mkoani Morogoro ataachiwa huru baada ya Mahakama Kuu ya
Tanzania Kanda ya Dar es Salaam kutengua hukumu aliyekuwa amehukumiwa na
Mahakama ya Wilaya ya Kilombero.
Peter
Ambrose Lijualikali alihukumiwa kwenda jela kwa kipindi cha miezi sita
baada ya kupatikana na hatia ya kufanya vurugu kipindi cha uchaguzi
mdogo mkoani humo.
Mbunge
huyo alifanya kosa hilo kipindi cha uchaguzi wa Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero mwezi Machi 2016 ambapo upinzani
walilalamikia uchaguzi huo kuwa ulijawa vurugu na vitisho vya polisi.
Polisi
walimkamata Mbunge huyo baada ya kudaiwa kuwa alitaka kuingia katika
chumba cha kupigia kura wakati yeye hakuwa na haki ya kupigakura.
Mahakama
Kilombero ilimhukumu mbunge huyo kifungo cha miezi sita jela lakini leo
Mahakama Kuu imetengua hukumu hiyo baada ya mbunge huyo kuto kukutwa na
hatia, na hivyo mbunge huyo ataachiwa huru.