Chama
cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza majina ya wanachama wake 12
walioteuliwa kugombea ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki, uchaguzi
unaotarajiwa kufanyika kwenye mkutano wa Bunge ujao.
Akisoma
majina hayo leo wakati wa Mkutano na waandishi wa habari, Katibu wa
Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema kuwa wameteua
wananchama hao miongoni mwa wengi zaidi ya 400 waliokuwa wamechukua fomu
kugombea nafasi hizo.
Mchanganuo
Miongoni
mwa wabunge 9 watakaokwenda Bunge la Afrika Mashariki kuiwakilisha
Tanzania, 6 watatoka CCM. Kufuatia idadi, hiyo CCM imesema kuwa itatoa
wabunge watatu wa kiume na watatu wa kike ambapo miongoni mwao wanne
watatokea Tanzania Bara na wawili watatokea Tanzania Visiwani.
Walioteuliwa kugombea nafasi hizo ni;
Wanawake Tanzania Bara;
- Zainabu Rashid Mafaume Kawawa
- Happiness Elias Lugiko
- Fancy Haji Nkuhi
- Happiness Ngoti Mgalula
Wanaume Tanzania Bara;
- Dkt Ngwaru Jumanne Maghembe
- Adam Omari Kimbisa
- Anamringi Issay Macha
- Charles Makongoro Nyerere
Wanawake Zanzibar;
- Maryam Ussi Yahya
- Rabia Abdallah Hamid
Wanaume Zanzibar;
- Abdallah Hasnu Makame
- Mohammed Yussuf Nuh
Miongoni
wa wagombea hawa 12, Bunge litapiga kura kuchagua wabunge sita
watakaoiwakilisha Tanzania kwenye Bunge la Afrika Mashariki kwa tiketi
ya CCM.