Katika
Mkoa wa Simiyu kumefanyika Mkutano Mkuu wa wadau wa Mfumo wa Bima ya
afya nchini (NHIF), Mkutano ulioongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko
huo Nchini Anne Makinda ambaye ni Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania pamoja na Mkuu wa mkoa huo Antony Mtaka.
Akongea
wakati wa Mkutano huo Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko huo, alionekana
kukerwa na uwepo wa baadhi ya watoa huduma kutoka katika zahanati, vituo
vya afya pamoja na hospitali nchini kutoa lugha chafu kwa wagonjwa na
kusababisha kuwepo kwa malalamiko mengi juu ya mfuko huo.
Mbali
na hilo Mwenyekiti huyo alikerwa kwa baadhi ya watoa huduma wa serikali
pamoja na watu binafsi, kukidhiri kwa udanganyifu wa madai kwenda NHIF,
ambapo alisema wengi wao wamekuwa wakipeleka madai hewa katika mfuko huo
kwa ajili ya kulipwa.
" hii
ni changamoto kubwa sana kwa watoa huduma wetu, wamekuwa wakituletea
madai ambayo siyo halisi, na kuashiria kuwepo kwa vitendo vya rushwa kwa
baadhi yao, jambo hili limekuwa kero kubwa sana mfuko na, hivyo ni
lazima wachukuliwe katua kuanzia ngazi za halmshauri na mikoa" Alisema
Mkutano
huo umeshirikisha wadau wengi wakiwemo viongozi wa kisiasa, wabunge,
Madiwani, wenyeviti wa halmashauri, wakuu wa wilaya, wakurugenzi,
wahuduma wa afya, watoa huduma binasfi, viongozi wa dini, walimu,
watumishi wa serikali kutoka idara mbalimbali, pamoja na wananchi.
Wakichangia
mada mbalimbali wadau wengi wamelalamikia changamoto ya ukosefu wa dawa
kwenye sehemu za kutolea huduma, licha ya kuchangia mfuko huo kila
mwaka, lucha chafu kutoka kwa baadhi ya wahudumu wa afya.
"
tumekuwa tukitumia muda wetu na wananchi wanatusikiliza na kutuunga
mkono kuchangia mfuko huu, lakini malalamiko yamekuwa mengi sana,
ukosefu wa dawa pamoja na lugha chafu, hapo ndipo na sisi tunavunjika
moyo na hali ya kuendelea kuchangia maana kila tukienda kuhamasisha
tunakumbana na maswali hayo na tunakosa majibu" Alisema Makondeko
Mbali
na hilo wadau hao walilalamikia mamlaka ya dawa nchini (Msd) kwa
kushindwa kutoa dawa za kutosha kwa vituo mbalimbali vya afya nchini,
ambapo baadhi waliiomba serikali kuifuta Msd, na kuunda chombo kipya
kutokana na kushindwa kazi, huku halmashauri zikiomba kuruhusiwa kununua
dawa moja kwa moja bila ya kupitia msd.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) ambaye pia ni Spika msaafu wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda, akiongea wakati
wa Mkutano Mkuu wa wadau wa Mfuko huo Mkoa wa Simiyu, mkutano
uliofanyika Mjini Bariadi katika Kanisa Katoliki Bariadi.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka akifungua Mkutano mkuu wa wadau wa mfuko
wa Bima ya afya (NHIF) uliofanyika leo mjini Bariadi katika kanisa
katoliki, ambapo Mkuu huyo wa Mkoa alitoa onyo kali kwa watoa huduma
katika mkoa huo binafsi pamoja na serikali kuacha mara moja tabia ya
kupeleka madai yasiyo halisi NHIF kwa ajili ya malipo.
Wadau mbalimbali katika Mkutano huo.
Wadau mbalimbali katika Mkutano huo.
Katibu
wa Itikadi na uenezi chama cha mapinduzi mkoa wa Simiyu (CCM) Geremia
Makondeko akichangia mada wakati wa Mkutano mkuu wa wadau wa mfuko wa
bima ya afya mkoani humo, mkutano uliofanyikia katika ukumbi wa kanisa
katoliki mjini Bariadi.
Kaimu
Mkurugenzi wa Mfuko wa Bima ya afya Nchini (NHIF) Bernard Konga, akitoa
taarifa ya mfuko huo, wakati wa mkutano mkuu wa wadau wa NHIF mkoa wa
Simiyu, ulifanyika leo katika kanisa katoliki Mjini Bariadi.
Meneja
wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) mkoa wa Simiyu, Amani Emmanuel akitoa
taarifa ya mfuko huo ya mkoa wa Simiyu, wakati wa Mkutano Mkuu wa wadau
wa NHIF mkoani humo, mkutano uliofanyikia katika ukumbi wa kanisa
katoliki mjini Bariadi.
Kaimu
Mkurugenzi wa Mfuko wa Bima ya afya Nchini (NHIF) Bernard Konga, akitoa
taarifa ya mfuko huo, wakati wa mkutano mkuu wa wadau wa NHIF mkoa wa
Simiyu, ulifanyika leo katika kanisa katoliki Mjini Bariadi.
Wadau wakifuatilia mada wakati wa mkutano huo.
Wadau wakifuatilia mada wakati wa mkutano huo.
Wadau wakifuatilia mada wakati wa mkutano huo.
Mwenyekiti
wa Bodi ya mfuko wa Bima ya afya Tanzania (NHIF) Anna Makinda (kushoto)
akiwa katika Mkutano wa wadau wa mfumo wa bima ya afya Mkoani Simiyu,
(kulia) ni Mkuu wa Mkoa huo Antony Mtaka.
Wadau mbalimbali walioshiriki wakiwemo viongozi wa Dini, (wa kwanza kushoto) Shekhe wa mkoa wa Simiyu Mohamud Kalokola.