Ikiwa
imepita miezi mitatu na siku kadhaa toka kutokea kwa tetemeko la Ardhi
mkoani Kagera leo Rais wa Jamhuri wa Muungano Mh. John Pombe Magufuli
anategemewa kuwasili mkoani humo kwa ziara ya siku mbili yenye lengo la
kuwatembelea wananchi
walioathirika na tetemeko la Ardhi lakini pia kuzindua na kuweka mawe
ya msingi katika miradi kadhaa ya maendeleo ambayo yaliathiriwa kutokana
na tetemeko hilo mkoani humo.
Mkuu
wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mstapha jana alisema Rais
ataingia asubuhi ya leo akitokea Geita na baadaye atahudhuria ibada ya
misa na kesho yake ndiyo atawatembelea baadhi ya wananchi waliotumia
nguvu zao kujenga nyumba zao na makazi baada ya kuharibiwa na tetemeko
la Ardhi kisha atatembelea miradi ya ujenzi wa shule ya Sekondari ua
Ihungo na kuweka jiwe la msingi na kuzungumza na wananchi.