Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Ramo Makani amesema kuwa hakuna mwenye
Mamlaka ya kutoa tamko au ufafanuzi kuhusu faru John kwa sasa zaidi ya
Waziri Mkuu kwa kuwa jambo hilo liko chini ya ofisi yake. kwaajili ya
uchunguzi.
Ameyasema
hayo Wilayani Ngorongoro katika ziara yake ya kikazi ya siku mbili
wilayani humo kufuatilia changamoto za uhifadhi pamoja na utekelezaji wa
maagizo ya Waziri Mkuu aliyo yatoa hivi karibuni akiwa Arusha.
“Ripoti
hii ya uchunguzi ni mali ya Waziri Mkuu atakae weza kutoa ripoti hii
nje kwaajili ya matumizi ya kila mmoja wetu kwa maana ya mamlaka, kwa
hiyo hakuna mamlaka nyingine ya serikali yenye uhalali wa kutoa tamko au
ufafanuzi wa jambo hili.”amesema Makani.
Hata
hivyo, Makani amesema kuwa wanasubiri maagizo au maelekezo na mwelekeo
wa sasa juu ya jambo hilo kutoka ofisi ya Waziri Mkuu.