Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
pamoja na balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke (kushoto) wakiweka
jiwe la msingi katika ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Ihungo
mkoani Kagera. Shule hiyo inajengwa upya kufatia kuathirika na tetemeko
la Ardhi lililotokea mkoani humo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitazama
wakati Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke alipokuwa akibonyeza
kitufe kuashiria uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya
Wavulana Ihungo mkoani Kagera. Wakwanza kushoto ni Waziri wa Elimu
Profesa Joyce Ndalichako.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
Balozi wa uingereza hapa nchi Sarah Cooke wakikagua ujenzi wa majengo ya
Shule ya Sekondari ya Wavulana Ihungo mkoani Kagera.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Majengo nchini (TBA) Elius Mwakalinga akitoa maelezo
ya mradi huo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli wakati wa ukaguzi.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Majengo nchini Elius Mwakalinga akitoa maelezo ya
mradi huo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli wakati wa ukaguzi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na Charles Masinde mmoja wa wanachi mkoani Kagera aliyeamua kujenga
nyumba yake mwenyewe mara baada ya tetemeko. Rais Dkt. Magufuli
amemuahidi mwananchi huyo kuwa atampatia mabati 30 kwa ajili ya kuezekea
nyumba yake.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifafanua
jambo wakati alipokuwa akikagua majengo ya shule ya Sekonadri ya
Wavulana Ihungo ambayo yanajengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).