Wajumbe
wa Jopo la Kuamua Mshindi wa Urais nchini Marekani wamemuidhinisha
Donald Trump kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Novemba.Hii
ni licha ya juhudi za dakika za mwisho za kutaka kumzuia kuingia ikulu
ya White House mwezi Januari.
Wiki
sita baada ya uchaguzi mkuu kufanyika tarehe 8 Novemba, mwanachama huyo
wa Republican amepata zaidi ya kura 270 za wajumbe ambazo alikuwa
anahitaji kufanya rasmi ushindi wake.