TUNDU Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kituo Kikuu cha Kanda Maalumu ya Dar es Salaam
“Nashikiliwa
na polisi hapa Kituo Kikuu kutokana na ile press conference (mkutano na
waandishi wa habari) kuhusu kupotea kwa Ben Saanane,” alimweleza mwandishi wa habari hii kupitia simu leo.
Mwandishi
alimtafuta Lissu kutaka kujua baadhi ya mambo, ndipo alipopokea simu na
kueleza hivyo. Hakuna taarifa zaidi mpaka sasa.
Saanane
ambaye ni Msaidizi wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa-Freeman Mbowe
alipotea ghafla takribani mwezi mmoja sasa na hajulikani alipo.
Wafuasi
wa CHADEMA wamekuwa wakimsaka kiongozi huyo bila mafanikio yoyote jambo
ambalo limeendelea kuzua hofu kama yu hai ama ameuawa.
Tarehe
14 Desemba mwaka huu, Lissu alizungumza na waandishi wa habari katika
Makao Makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam akiomba
vyombo vya ulinzi kusaidia kupatikana kwa kiongozi huyo.
Chanzo: Mwanahalisi