Ajira hii ni kwa walimu wa stashahada na
shahada za mafunzo ya ualimu wa masomo ya hisabati na sayansi,
waliohitimu mwaka 2015. wahitimu hao wanatakiwa kuwasilisha nakala za
vyeti vyao vya elimu ya sekondari (kidato cha nne na sita) na taaluma ya
ualimu (stashahada na shahada) kwa ajili ya uhakiki.
Nakala hizo ziwasilishwe kupitia barua pepe ya wizara info@moe.go.tz kuanzia tarehe ya tangazo hili hadi ijumaa tarehe 16/12/2016.
yeyote ambaye vyeti vyake havitahakikiwa hatafikiriwa katika uajiri.
Tangazo hili linapatikana pia kwenye tovuti za ofisi zifuatazo: OR-TAMISEMI, NECTA, TCU na NACTE.
imetolewa na:
Katibu Mkuu
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia