SERIKALI
imetangaza kuajiri walimu wa masomo ya sayansi na hisabati katika shule
za sekondari ambao wametakiwa kupeleka nakala za vyeti vyao vya elimu
ya sekondari, vya taaluma ya ualimu (stashahada na shahada) kwa ajili ya
uhakiki.
Tangazo
kwa Umma lililotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia, Maimuna Tarish lilisema vyeti vya sekondari vinavyotakiwa
kuhakikiwa ni vya kidato cha sita.
Alisema
ajira hizo ni kwa walimu wa Stashahada na Shahada za Mafunzo ya Ualimu
wa Masomo ya Hisabati na Sayansi waliohitimu mwaka 2015.
Alisema
nakala hizo ziwasilishwe kupitia barua pepe ya wizara kuanzia jana hadi
Ijumaa ya Desemba 16 mwaka huu na yeyote ambaye vyeti vyake
havitahakikiwa hatafikiriwa katika uajiri.