Mkuu
wa Wilaya ya Ubungo, Humphrey PolePole ameteuliwa na Halmashauri Kuu ya
Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu
Itikadi na Uenezi kuchukua nafasi ya Nape Nnauye
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na chama hicho kupitia ukurasa wake wa
Twitter zinaeleza kuwa kikao chaHalmashauri Kuu ya Taifa kimemteua
Polepole kushika wadhifa huo.
Kikao
cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kimefanyika leo ambapo miongoni mwa
mambo mengi yatakayojadiliwa ni pamoja na tathmini ya uchaguzi mkuu wa
mwaka 2015.