test

Jumapili, 22 Oktoba 2017

Licha Ya Kukabiliwa Kesi Ya Mauaji Na Kuwa Uwezekano Wa Kufungwa...LULU atangaza Ndoa Na Huyu Hapa


Baba mzazi wa msanii wa filamu Bongo Elizabeth Michael ‘Lulu’, Mzee Kimemeta amefunguka mambo kadhaa kuhusu mwanaye kuolewa.

Akizungumza na East Africa Radio, Mzee Kimemeta amesema kwanza hana shinikizo kwa mwanaye aolewe na mtu fulani kwa sababu ni maarufu bali ni maamuzi yake binafsi na suala la posa kwake halipo.
“Suala la kuoana mimi halinihusu ni suala la watu wawili, anayeoa na anayeolewa, yeyote atakayemleta akaniambai baba huyo ndio wangu sisi tunambariki” amesema.
“Hapa, sisi kwa kweli posi haipo katika msamiati wangu, siuzi mtoto wala sitaki posa yoyote, posa yangu ni amani ndani ya nyumba yao, ndio posa watakayoniletea,” amemaliza kwa kusema.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni