Jumapili
Disemba 18 mwanamuziki Darassa akiwa na mtayarishaji wa muziki, Abbah
pamoja na mtayarishaji wa video za muziki, Hanscana walipata ajali
Kahama mkoani Shinyanga walipokuwa njiani kurejea Dar es Salaam.
Katika ajali hiyo ambapo Darassa ndiye alikuwa dereva, wote walinusurika kifo lakini wakiwa na majeraha machache.
Baada ya kufika Dar es Salaam, Darassa alikwenda Hospitali ya Taifa
Muhimbili kwa ajli ya matibabu na baada ya kufanyiwa vipimo, alitakiwa
kupumzika kwa muda bila kufanyama matamasha ya muziki au shughuli
nyingine ngumu ili aweze kupona majeraha madogo aliyoyapata.
Picha: Mwanamuziki Darassa apata ajali Kahama
Kupitia CloudsFm leo Darassa amesema kuwa “Nipo hospitalini Muhimbili
sasa hivi nawashukuru sana madaktari wa hapa wamenipokea vizuri wamenipa
huduma nzuri sana, wamenicheki kwa sababu nilikuwa najisikia vibaya
sana sehemu za kichwani nashukuru Mungu majibu yanaonyesha kila kitu
kipo poa kabisa kuna damage ndogo wanaifanyia kazi naendelea na matibabu
ila nimeshauriwa kupunguza mizunguko kwa wiki moja ili niweze kupumzika
na kutibu hayo maumivu ya kichwa.”
Darassa ni mwanamuziki anayetamba zaidi kwa sasa nchini Tanzania na
wimbo wake wa Muziki aliomshirikisha Ben Pol ambao umekuwa ukishangiliwa
popote pale unaposikika.