December
18 Rapa Darassa aliripotiwa kupata ajali akiwa safarini kutokea Kahama
ambako alikua na show wikiendi iliyopita, Jeshi la Polisi Tanzania
kupitia mkoa wa Shinyanga wametoa taarifa ya ajali hiyo ikiwemo chanzo
chake cha ajali.
Abbah, Mr Vs, Darassa na Hanscana wote wame nusurika kwenye ajali hiyo
TAARIFA YA JESHI LA POLISI (M) SHINYANGA KWA VYOMBO VYA HABARI. 18/12/2016
AJALI
YA GARI KUACHA NJIA , KUPINDUKA, KUSABABISHA MAJERUHI NA UHARIBIFU WA
GARI. TAREHE 18/12/016 SAA 15:00, HUKO KATIKA KIJIJI CHA NTOBO, KATA YA
NTOBO, TARAFA YA MSALALA , (W) YA KAHAMA MKOA WA SHINYANGA, GARI REG NO T
503 DGQ TOYOTA DARK BLUE HARRIER MALI YA SHARIF S/O THABIT RAMADHAN
@DARASSA BOXDSM, MNYAMWEZI ,MIAKA 28 , IKIENDESHWA NA YEYE MWENYEWE
ILIACHA NJIA, KUPINDUKA NA KUSABABISHA MAJERAHA KWA SWITBERT S/O CHARLES
,MSUKUMA ,MIAKA 24 , PRODUCER WA MUZIKI, MKAZI WA DSM AMBAYE AMEPATA
MICHUBUKO MIKONO YOTE MIWILI, PIA KUSABABISHA UHARIBIFU MKUBWA WA GARI
HILO. MAJERUHI AMETIBIWA KITUO CHA AFYA CHA MGODI WA DHAHABU BULYANHULU
NA HALI YAKE INAENDELEA VIZURI .CHANZO CHA AJALI HIYO NI MWENDO KASI WA
DEREVA WA GARI HILO. HATUA ZINGINE ZA KISHERIA ZITAFUATA.. RPC
SHINYANGA.
Kwamujibu
wa Bongo5 Jumatatu hii imeripoti kuwa, Hanscana amedai hajui chanzo
cha ajali hiyo huku akidai hata yeye anashangaa kwani walikuwa kwenye
mwendo wa kawaida sana.
“Dereva
alikuwa Darassa wakati tunapata ajali na kusema kweli tulikuwa kwenye
mwendo wa kawaida sana, ghafla tukashangaa kuona gari ina serereka na
kupinduka mara nne. Kwa hiyo ni ajali kama ajali nyingine sema sisi
tunashangaa mazingira ya ajali lakini yote ya yote tunamshuru Mungu kwa
sababu wote ni wazima,” alisema Hanscana.
Aliongeza, “Kwa
sasa tunaangalia namna gani tunaweza kurudi Dar es salaam kwa sababu
huku tuliko ni mbali sana na tulikuja kwa ajili ya show,”.
Hizi ni baadhi ya picha kutoka kwenye Ajali hiyo siku ya Jana