“Kwa leo siwezi kuzungumza lolote kutokana na hali ilivyo, na namna jinsi watu wanavyoendelea kulizungumzia jambo hili lakini nitazungumza wakati ukifika na mtajua,” alisema
Dk Mwele kwa sauti ya uchangamfu.
Uteuzi wake ulitenguliwa Ijumaa usiku baada ya kutoa ripoti ya mwaka ya taasisi hiyo iliyoonyesha kuwa watu 80 waliofanyiwa utafiti waligundulika kuwa na virusi vya homa ya zika.
Taarifa ya utafiti huo ilionyesha kuwa kati ya watu 533 waliopimwa, 83 (asilimia15.6) walikuwa wameambukizwa virusi vya homa zika. Pia, kati ya watoto wachanga 80 waliozaliwa na ulemavu wa aina mbalimbali, asilimia 43.8 walikuwa wameambukizwa virusi vya homa ya zika.
VIDEO: Muigizaji Nisha bebee anywa mkojo wake kisa kumsahau mwanawake