Ndugu
zangu, nawashukuruni wote mliojaribu kunitafuta na kunipa pole toka
jana. Sikuwa napatikana kwa sababu walionivamia waliiba simu pamoja na
vitu vingine.
Kilichotokea: Usiku wa
saa tano siku ya Alhamisi (juzi) nilisimamishwa na gari baada kupigiwa
honi na kuwashiwa taa na gari iliyokuwa nyuma yangu. Niliposhusha kioo
driver akawa anaongea haraka haraka kwamba nimewagonga wakati narudi
nyuma parking na nakimbia. Nikamjibu kwamba sijamgonga.
Akaniambia umetugonga
angalia bampa. Kweli bampa lilikuwa limelegea. Ila sikuwa nimewagonga
hivyo nikaendelea kubisha. Akaniambia shuka uangalie hata pembeni.
Alikuwa amevaa smart tu so nikashuka. Wakati naangalia anaposema
nimemgonga wakashuka wengine wawili kutoka kwenye gari na kunishika.
Wakaanza kunishambulia huku wakinipora wallet, saa nk. Then wakanikata
panga kichwani na kupekua gari wakaondoka na laptop na simu pamoja na
funguo wa gari.
Kwa sasa naendelea vizuri baada ya kupata matibabu. Nawashukuru wote.
Albert Msando