Halmashauri
Kuu ya Taifa ya CCM imekutana leo tarehe 13/12/2016 jijini Dar es
salaam kwa kikao cha siku moja cha kawaida. Kikao hicho kimeongozwa na
Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli.
Pamoja
na mambo mengine, Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imepokea taarifa ya
Tathimini ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, baada ya kuitafakari taarifa
hiyo, Halmashauri Kuu imeamua yafuatayo;-
1.
Kupunguza idadi ya wajumbe wa vikao na idadi ya vikao vya Chama katika
ngazi mbalimbali ili kuongeza ufanisi wa utendaji wa Chama na kuongeza
muda wa viongozi wa Chama kufanya kazi za Chama kwa Umma badala ya
kutumia muda mwingi vikaoni.
Ili kuwa na vikao vya Chama vyenye tija imeamuliwa kama ifuatavyo:-
a).
Halmashauri Kuu ya Taifa kwa sasa ina jumla ya wajumbe 388 idadi ambayo
ni kubwa sana, hivyo imeamuliwa idadi hii ipunguzwe na kuwa wajumbe 158
kama ifuatavyo:-
Wenyeviti wa Mikoa
Mikoa ya Bara 26x1 = 26
Mikoa ya Zanzibar 6x1 = 6
Wajumbe wa NEC wa Mikoa
Mikoa ya Bara 26x1 = 26
Mikoa ya Zanzibar 6x4 = 24
Wajumbe wa NEC wa Taifa
Kutoka Bara = 15
Kutoka Zanzibar = 15
Nafasi za Mwenyekiti = 7
Wajumbe wa NEC wa Jumuiya
UVCCM = 5
UWT = 5
WAZAZI = 5
Wajumbe wa NEC kutoka Bungeni = 5
Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CCM = 1
Wajumbe wa NEC kutoka BLW = 3
Katibu wa Kamati ya Wawakilishi = 1
Wajumbe wa NEC – wanaotokana na Nyadhifa zao
- Mwenyekiti wa CCM = 1
- Makamu Mwenyekiti (B) = 1
-Makamu Mwenyekiti (Z) = 1
- Makamu wa Rais = 1
- Waziri Mkuu = 1
- Makamu wa Pili wa Rais (Z) = 1
- Spika wa Bunge = 1
- Spika wa BLW = 1
- Mwenyekiti wa UWT = 1
- Mwenyekiti wa WAZAZI = 1
-Mwenyekiti wa UVCCM = 1
- Katibu Mkuu – WAZAZI = 1
- Katibu Mkuu – UWT = 1
- Katibu Mkuu – UVCCM = 1
Jumla: 158
#.
Vikao vya kawaida vya Halmashauri Kuu ya Taifa vifanyike kila baada ya
miezi sita badala ya miezi minne kama ilivyo sasa isipokuwa vinaweza
kufanyika vikao maalum inapohitajika.
b). Kwa upande wa sasa imeamuliwa wajumbe wa Kamati Kuu wawe 24 badala ya 34 kama ifuatavyo:-
Mwenyekiti wa CCM.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara)
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar)
Makamu wa Rais
Katibu Mkuu wa CCM
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara)
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar)
Waziri Mkuu
Makamu wa Pili wa Rais (Z)
Spika wa Bunge la Tanzania
Spika wa BWL
Mwenyekiti wa WAZAZI
Mwenyekiti wa UWT
Mwenyekiti wa UVCCM
Katibu wa wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Organaizesheni
Katibu wa wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Itikadi na Uenezi
Katibu wa wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Uchumi na Fedha
Katibu wa wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa
Wajumbe watatu (3) wa kuchaguliwa na Halmashauri Kuu kutoka Tanzania
Wajumbe watatu (3) wa kuchaguliwa na Halmashauri Kuu kutoka Zanzibar.
#.
Vikao vya kawaida vya Kamati Kuu vipunguzwe ili vifanyike kila baada
ya miezi minne badala ya miezi miwili isipokuwa vinaweza kufanyika vikao
maalum inapohitajika.
c). Kwa ngazi ya mkoa, Wajumbe wa Kamati za Siasa za Mikoa wapunguzwe kwa kuondoa wajumbe watatu ambao ni:-
Katibu wa Uchumi na Fedha wa Mkoa - 1
Wajumbe wa kuchaguliwa na H/Mkoa - 2
#.
Vikao vya kawaida vya Kamati ya Siasa ya Mkoa vifanyike kila baada ya
miezi mitatu badala ya kila mwezi kama ilivyo sasa isipokuwa vinaweza
kufanyika vikao maalum inapohitajika.
d). Kwa upande wa Wilaya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya wapunguzwe kwa kuwoandoa:-
Katibu wa Uchumi na Fedha wa Wilaya - 1
Katibu wa Kamati ya Madiwani - 1
Wajumbe wa kuchaguliwa na H/Kuu ya (W)- 2
Jumla: 4
#.Vikao
vya kawaida vya Kamati ya Siasa ya Wilaya vifanyike kila baada ya
miezi mitatu badala ya kila mwezi isipokuwa vinaweza kufanyika vikao
maalum inapohitajika.
#. Muundo wa Wilaya za Chama uendane na muundo wa sasa wa Serikali.
Kata,Tawi na Shina
Idadi ya kuanzisha Shina iwe wanachama 50 hadi 300.
Idadi ya kuanzisha Tawi iwe wanachama kuanzia 301 hadi 1,000.
Hata hivyo idadi hii izingatie eneo la kijiografia na wingi wa wanachama katika eneo hilo.
Vikao
vya kawaida vya Kamati za Siasa za ngazi hizi viwe vinafanyika mara
moja kila baada ya miezi mitatu, isipokuwa vinaweza kufanyika vikao
maalum inapohitajika.
#. Nafasi za Uongozi
Mwanachama
anatakiwa kuwa na nafasi moja tu ya uongozi wa kazi za muda wote kama
ilivyoainishwa kwenye Kanuni za uchaguzi wa Chama Toleo la 2012 kifungu
cha 22 na 23 ambazo zimetajwa kuwa ni:-
Mwenyekiti wa Tawi,Kijiji au Mitaa.
Mwenyekiti wa Kata/Wadi.
Mwenyekiti wa Jimbo, Wilaya na Mkoa.
Makatibu wa Halmashauri Kuu wa ngazi zote zinazohusika.
Mbunge, Mwakilishi na Diwani.
#.
Viongozi wa kuchaguliwa waepuke kuwa watendaji badala yake waongoze na
kusimamia shughuli za Chama kwa kuzingatia Katiba na Kanuni.
#.Vyeo ambavyo haviko kwenye Katiba
Vyeo
ambavyo havijatamkwa kwenye Katiba ya CCM haviruhusiwi katika Chama au
Jumuiya zake mfano Umoja wa makundi mbalimbali kama Wenyeviti wa ngazi
mbalimbali (mfano: Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM n.k), Makamanda
(UVCCM), Washauri (UWT) na Walezi (WAZAZI) katika ngazi zote.
#. Uhakiki wa Wanachama wa CCM
Halmashauri
Kuu imeona ipo haja ya kufanya uhakiki wa wanachama wa CCM na Jumuiya
zake ili kujua idadi sahihi ya wanachama wetu kwa wakati huu. Uhakiki
huu uendane na kutoa kadi mpya za uanachama za kielektroniki ili kuwa na
udhibiti wa usahihi wa wanachama na kuondoa wanachama HEWA. Aidha, Kadi
za UWT, WAZAZI na UVCCM zifutwe ili tubaki na kadi za CCM tu.
#. Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi
Jumuiya
za CCM zimetakiwa kufanya kazi zake kwa kuzingatia matakwa ya Katiba
ya CCM na Kanuni za Jumuiya husika, kanuni za Jumuiya ziendane na
matakwa ya Katiba ya CCM.
#.Uaendeshaji
wa shughuli zote za Jumuiya za Chama na mali zake uwe chini ya
usimamizi wa Chama Cha Mapinduzi. (Baraza la Wadhamini la Chama Cha
Mapinduzi).
Makatibu
Wakuu wa Jumuiya watakuwa wanateuliwa na Kamati Kuu na Manaibu Katibu
Wakuu watateuliwa na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa.
#.
Wakati tukiendelea kubaki na Bendera yenye rangi ya kijani na njano
na alama ya jembe na nyundo, Halmashauri Kuu imeona ipo haja ya
kuzifanya rangi hizo kuwa na muenekano wa kuvutia zaidi.
#.
Utumishi katika Chama na Jumuiya zake. Katibu Mkuu wa CCM na
Sekretarieti ipewe majukumu ya kusimamia ajira za Watumishi wa Chama na
Jumuiya zake.
Nafasi
za Makatibu Wasaidizi wa Mikoa na Wilaya zitaondolewa na badala yake
kazi zao zitatekelezwa na Makatibu wa Jumuiya za Chama wa Mikoa na
Wilaya kwa utaratibu utakaopangwa. Utaratibu huu utakipunguzia Chama
Cha Mapinduzi gharama na kujenga umoja wa utendaji kazi wa Chama na
Jumuiya zake katika Mikoa na Wilaya.
#. Tathimini ya hali ya Kisiasa na Uchaguzi wa Zanzibar .
Halmashauri
Kuu ya Taifa imeagiza kuundwa kwa Kamati maalum ya kufanya tathimini ya
kina kuhusu hali ya kisiasa Zanzibar kwa ujumla na masuala yanayohusu
uchaguzi wa Zanzibar 2015.
#
Mwenyekiti wa Kamati ya udhibiti na nidhamu ametakiwa akamilishe kazi
ya taarifa ya udhibiti kwa wanachama waliokiuka mienendo ya kiuanachama
kabla ya kuanza uchaguzi Mkuu wa Chama mwezi Februari 2017, Mikoa na
Wilaya ambazo hazijaleta taarifa zao za kiudhibiti ziwe zimefikisha
taarifa zao kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Udhibiti na Nidhamu kabla ya
tarehe 30/01/2017.
#.
Uhakiki wa Mali za Chama uendelee kufanyika kwa kina na uchambuzi zaidi
ukikamilika Taarifa yake iwasilishwe kwa Sekretarieti ya Halmashauri
Kuu ya Taifa mapema iwezekanavyo.
#. Maamuzi na mapendekezo haya yatapelekea kufanyika kwa mabadiliko ya Katiba ya Chama na Kanuni za Jumuiya za Chama.
#.
Kwa mambo yale ambayo yatahitaji mabadiliko ya Katiba, Mkutano Mkuu
utaandaliwa mapema mwakani na kutafakari na kupitisha mabadiliko hayo ya
Katiba.
Mwenyekiti wa CCM Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ameteua wafuatao kujaza nafasi mbalimbali ndani ya sekretarieti ambazo zimekuwa wazi kutokana na waliokuwa wakizishikilia kupewa majukumu mengine ya kiserikali.
#.Ndg.
Rodrick Mpogolo anakuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara kuchukua nafasi
iliyoachwa wazi na Ndg. Rajabu Luhwavi ambaye ameteuliwa kuwa balozi.
#.
Col. Ngemela Eslom Lubinga- Kuwa Katibu NEC Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Dr. Asha-Rose Migiro
aliyeteuliwa kuwa Balozi
#.
Humphrey Polepole kuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi kujaza nafasi
iliyoachwa wazi na Ndg. Nape Nnauye aliyeteuliwa kuwa Waziri.
#. Wajumbe wengine watabaki kama walivyo sasa.
Imetolewa na:-
NAPE NNAUYE
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
13/12/2016