BARACK OBAMA
Rais wa Marekani aligonga vichwa vya habari alipotokwa
na machozi alipokuwa akiwahimiza Wamarekani
wakubali mabadiliko kwenye masharti ya uuzaji wa
silaha Marekani.
Alizidiwa na hisia alipokuwa akisimulia kuhusu
shambulio la ufyatuaji risasi katika shule ya msingi ya
Sandy Hook mwaka 2012 ambapo watoto 20 na watu
wazima sita.
Hii haikuwa mara yake ya kwanza kutokwa na machozi
akizungumzia kisa hicho.
HAMID KARZAI
Rais wa zamani wa Hamid Karzai aligonga vichwa vya
habari duniani alipolia kuhusu hali ya Afghannistan
wakati wa kutoa hotuba katika shule ya upili ya Kabul
Septemba mwaka 2010.
Alitokwa na machozi alipokuwa akizungumzia mapigano
nchini mwake, akisema alikuwa na wasiwasi kwamba
hilo lingemfanya mwanawe kutorokea ng’ambo.
LUIZ INACIO LULA DA SILVA
Rais wa zamani wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva
anajulikana pia kwa kutokwa na machozi hadharani.
Alibubujikwa na machozi mwaka 2009 baada ya mji wa
Rio de Janeiro kutangazwa kwamba ungekuwa mwenyeji
wa Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2016.
Machozi yake hayakuathiri umaarufu wake na ni mmoja
wa marais waliopendwa sana katika historia ya aifa hilo.
RYUTARO NONOMURA
Video ya mwanasiasa wa Japan aliyelia baada ya
kuulizwa maswali na wanahabari kuhusu matumizi yake
ya pesa ilivuma sana mtandaoni Julai 2014.
Ryutaro Nonomura alitokwa na machozi alipotakiwa
kujibu madai kwamba alikuwa ametumia pesa za umma
kwa safari za kibinafsi.
Alisisitiza kwamba zilikuwa ziara za kikazi,na Baadaye
alijiuzulu