test

Jumanne, 1 Novemba 2016

Upigaji kura Tuzo ya Mtu Mashuhuri Afrika 2016 umefungwa rasmi, Rais Magufuli aongoza kwa 84%


Zoezi la upigaji kura kwenye Tuzo ya Mtu Mashuhuri Barani Afrika kwa mwaka 2016 limefungwa rasmi Tarehe 1 Novemba 2016 saa Sita Kamili Usiku. Hadi zoezi hilo linafungwa, Rais Magufuli anaongoza kwa kupata asilimia 84 akifuatiwa kwa mbali na Watu wa Rwanda wenye asilimia 12.Nichukue fursa hii kuwapongeza wale wote waliompigia kura Rais wetu. Niwape pia pole wale wote waliokuwa wanahamasishana kwenye Magroup yao ya facebook na Whatsapp ili wawapigie kwa wingi Wanyarwanda kwa lengo tu la kutaka Rais Magufuli akose tuzo hiyo.

Sasa ni dhahiri kwamba, Tuzo ya 2016 inarudi tena Tanzania baada ya mwaka 2015 kunyakuliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya METL, Mohamed Dewji.

Swali la kujiuliza, je Rais wetu atarudi tena Nairobi Novemba 17 kuchukua Tuzo hiyo? Binafsi natamani sana kuona Rais akipokea Tuzo hiyo Mwenyewe. Hata hivyo, anaweza pia kutuma mwakilishi kupokea kwa niaba yake kama kutakuwa na udhuru. Kikubwa zaidi ni kwamba Tuzo inakuja tena Tanzania.


image.jpgimage.jpgimage.jpg

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx