Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewaomba wakazi wa Kagera walioathirika na tetemeko kufanya jitihada za kujijengea nyumba zao wenyewe kwani michango iliyochangwa na wadau imeelekezwa kwenye taasisi za serikali na kwamba hata michango itakayopatikana itaelekezwa kwenye makundi maalum.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera amedai kuwa jumla ya fedha zilizochangwa ni zaidi ya Bilioni 5.4 na kusema kuwa zimeelekezwa katika kukarabati miundombinu ya taasisi za Serikali na kuwataka wananchi wanaosubiri msaada wa serikali kusubiri mchango itakayotolewa na wadau walioahidi kuwasaidia waathirika moja kwa moja.