Mandamano ya jana yalitarajiwa kuwa makubwa zaidi yaliyowahi kutokea huku viongozi wa maandamano hayo wamesema mamilioni ya watu watashiriki huku wakiwa na nia ya kufika ikulu ya nchi hiyo.
Wakati huo huo serikali imewatuma maelfu ya maafisa wake wa polisi kwenye mji huo kwa ajili ya kukabiliana na ghasia za waandamanaji hao wanaopinga serikali.
Rais Hye anatuhumiwa kwa kuvujisha nyaraka za serikali kwa rafiki yake wa karibu anayefahamika kwa jina la Choi Soon-Sil ambaye alijaribu kuibia serikali fedha nyingi kupitia kampuni kadhaa za taifa hilo.
Hata hivyo Choi amekamatwa na kushtakiwa kwa ubadhirifu wa fedha za umma alizowahi kuziiba na kutumia vibaya mamlaka yake huku maafisa kadhaa waliopo kwenye ofisi ya Rais Guen wanachunguzwa dhidi ya sakata hilo.