Kocha huyo wa Man United amepigwa faini hiyo kufuatia kutoa maoni juu ya mwamuzi Anthony Taylor kabla ya mchezo wao dhidi ya Liverpool mwezi jana. Makocha huwa hawarusiwi kuwazungumzia waamuzi kabla ya mchezo.
Kocha huyo amefungiwa kukaa kwenye benchi kwa mechi moja kufuatia kutoa maneno mabaya kwa mwamuzi Mark Clattenburg katika mchezo dhidi ya Burnley jumamosi iliyoisha, kifungo hicho atakitumikia mechi ya jumapili hii dhidi ya Swansea.