test

Jumatatu, 28 Novemba 2016

MBUNGE WA CHALINZE RIDHIWANI AKABIDHI VISIMA VITATU VYENYE THAMANI YA SH.MILLION 84.5



Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, wa kushoto akiwa na Afisa Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali toka Nchini Omani linaloitwa TUELEKEZANE PEPONI Bw.Nasr Al Jahdhamy wakati wa kukabidhi visima vitatu kwa wananchi wa jimbo hilo.


Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, wa pili kutoka kushoto anayemfatia ni Afisa Mtendaji Bw.Nasr Al Jahdhamy mwakilishi kutoka Oman na Katibu wa Mbunge Bwana Swala na Mzee Maokola wakati wa kukabidhi visima vitatu kwa wananchi wa jimbo hilo.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, akiongea na wananchi wa jimbo hilo akiwa na Afisa Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali toka Nchini Omani linaloitwa TUELEKEZANE PEPONI Bw.Nasr Al Jahdhamy wakati wa kukabidhi visima vitatu kwa wananchi wa jimbo hilo.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, na Afisa Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali toka Nchini Omani linaloitwa TUELEKEZANE PEPONI Bw.Nasr Al Jahdhamy wakati wa kukabidhi visima vitatu kwa wananchi wa jimbo hilo wakiwa katika picha ya pamoja na na baadhi wa watoto jimbo hilo .



Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amekabidhiwa visima Vitatu vyenye thamani ya Shilingi Milioni 48.5 toka kwa Shirika lisilo la kiserikali toka Nchini Omani linaitwa kwa TUELEKEZANE PEPONI chini ya Afisa Mtendaji wake Nasr Al Jahdhamy.

Akizungumza wakati wa kukabidhi visima hivyo Mbunge huyo alisema kuwa , shida ya maji ndani ya Halmashauri ya chalinze imekuwa kubwa na kueleza kuwa kazi iliyofanyika kufanikisha ujenzi wa visima hivyo ni kubwa ili kusaidia tatizo hilo kwa kipindi hiki wakati wakisubiri kukamilika kwa ujenzi wa mradi wa kutoa maji mto wami. 

"Nimeona nifanye kazi ya kutengeneza visima ili kupunguza ukali wa uhaba wa maji kwani matengenezo ya mradi wa wami bado yanaendelea kuchimbwa kwa visima hivi si ishara kuwa ule mradi wa maji ambao tuliongea kuwa umekufa mradi wa wami utakapokamilika tunataraji utawanufaisha wananchi wengi wa jimbo letu."alisema Ridhiwani

Aidha visima hivyo vitatu vimekabidhiwa katika kijiji cha matipwili , shule ya sekondari ya matipwili na kijiji cha Gongo ambavyo vinaendelea kujengwa na vinataraji kukamilika mapema ndani ya wiki ijayo.

Naye Bwana Naseer aliahidi kuendelea kumsaidia Mbunge kufikia malengo yake ya kusaidia kutatua changamoto zinazokabili nyimbo hilo,na kuongeza kuwa atasaidia kuchimba visima vingine kumi katika Halmashauri hiyo na kusaidia michezo.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx