H.CLINTON (DEM) VS D.TRUMP (GOP)
Wanajamvi
Miaka , miezi, siku na ni masaa machache tu uchaguzi wa Marekani utakamilika.
Macho ya dunia yapo Marekani kujua nani atakuwa Rais ajaye wa Taifa hilo lenye nguvu
Uchaguzi wa Marekani unaathari kubwa kwa dunia. Ni taifa lenye nguvu za kiuchumi, kijeshi, kisiasa na kijamii zinazoathiri mataifa mengine. Kwa hali yoyote ni tukio linalogusa dunia
Hatua zote za uchaguzi zimefanyika na upigaji kura wa awali umeshamalizika
Kesho ni siku ya kupiga kura ambapo state zilizokuwa na uchaguzi wa awali zitamalizia na zile zinazofanya kea siku moja zitamaliza.
Itakapofika saa 3.0 usiku saa za Marekani sawa na saa 11 saa za Tanzania vituo vya mashariki vitafungwa. Vituo vya Marekani kati na magharibi vitafunga kwa muda huo kwa nyakati zao
Kwa kuangalia ramani ya uchaguzi na umuhimu wa Mjaimbo, matokeo yanaweza kukamilika ikifika saa 4 au 5 za Marekani kama hakutakuwa na tatizo ambazo ni sawa na saa 12 au 1 za Tz
Uzi huu utakuwa maalumu na endelevu ukiwaletea hali halisi ya matokeo kwa muda (real time)
Kutakuwa na uchambuzi wa kila tukio linalohusiana na uchaguzi kwa wakati.
Kura ya kwanza kabisa imepigwa katika kituo cha Dixville Notch, New Hampshire ambapo hadi kufikia saa tano mchana kwa saa za Tanzania Clinton anaongoza kwa kura 4 dhidi ya Trump kura mbili. Ni kawaida kwa kituo hiki kuwa cha kwanza kufungua milango ya kupigia kura toka mwaka 1960.
Nyote mnakaribishwa na uzi huu utakuwa 'active' kesho Jumanne saa 2 za usiku za Marekani sawa na saa 10 usiku Tz na kuendelea hadi matokeo ya mwisho
Hadi wakati huo endelea kuwa nasi Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA
Kaa mkao wa habari