Jeshi
la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na shughuli zake za kila siku ili
kuhakikisha mkoa unakuwa salama hii ni kutokana na wananchi kutoa
ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kuweza kuwabaini wahalifu wanaofanya
vitendo vya uhalifu ili mkoa wetu uwe salama.
Hata
kuanzia tarehe 01.11.2016 Jeshi la Polisi lilianza zoezi la ulinzi wa
Mitihani ya Kitaifa ya kuhitimu kidato cha nne 2016 katika Shule
mbalimbali za mkoa wa mbeya. Hata hivyo katika zoezi hilo linaloendelea
la ulinzi wa mitihani kuna changamoto zilijitokeza:-
KUFANYA KITENDO KIBAYA KINYUME NA MAADILI.
Mnamo
tarehe 04.11.2016 majira ya saa 23:30 usiku huko katika Shule ya
Sekondari Isuto iliyopo Kijiji na Kata ya Isuto, Tarafa ya Isangati,
Wilaya ya Kipolisi Mbalizi, Mkoa wa Mbeya, askari wawili wa Jeshi la
Polisi Mkoa wa Mbeya waliofahamika kwa majina ya 1. H.4925 PC PETRO
OSCAR MAGANA wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Mbeya na 2. J.1422 PC
LUKAS JOSEPH NG’WEINA wa Wilaya ya Kipolisi Mbalizi walituhumiwa
kuwafanyia vitendo vibaya kinyume na maadili wanafunzi wa kike wa kidato
cha nne wa Shule hiyo.
Inadaiwa
kuwa, askari hao kwa pamoja wakiwa kwenye ulinzi wa mitihani ya kitaifa
ya kidato cha nne 2016 waliwatoa kwenye Hostel wanafunzi wa kike kwa
kile walichodai kupiga kelele.
Baada
ya kuwatoa wanafunzi hao, waliwapeleka eneo la kufoleni na kuanza
kuwapa adhabu mbalimbali ambazo ni kupiga push up, kuruka kichura,
kushika masikio na kuwachapa viboko sehemu za makalio vitendo
vilivyowasababishia maumivu makali na kupelekea baadhi ya wanafunzi hao
wa kike kuondoa na kuelekea nyumbani kwao.
Kufuatia
vitendo hivyo, Mkuu wa Shule hiyo aitwaye ROSE MZEE DIHEMBE alitoa
taarifa kwa uongozi wa Wilaya ambapo taarifa zilifika kwa uongozi wa
Mkoa ambao mara moja walifika eneo la tukio na kuchukua hatua za awali
ikiwemo kusikiliza malalamikio hayo ya tukio na kuwaondoa askari
waliolalamikiwa na mwisho kuchukua hatua za kinidhamu zilizopelekea
kufukuzwa kazi askari hao.
Hata hivyo, kutokana na vitendo walivyovifanya askari hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.
WITO:
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishna wa Polisi DHAHIRI A. KIDAVASHARI
anatoa wito wananchi waendelee kuliamini Jeshi la Polisi kwamba
halitafumbia macho vitendo vya askari vinavyokwenda kinyume na maadili
ya kazi yao. Pia vitendo vinavyokwenda kinyume na sheria za nchi.
Aidha
Kamanda KIDAVASHARI anaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa ya vitendo
vyote vya uhalifu vinavyotendwa bila kujali vinatendwa na askari au
wananchi wa kawaida ili hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa.
Imesainiwa na:
[DHAHIRI A. KIDAVASHARI – DCP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.