Mkuu wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Simon Siro amesema kuwa jeshi la polisi linaendelea na oparesheni juu ya matumizi ya shisha huku watu watatu wa wilaya Kinondoni wakishikiliwa kwa matumizi ya madawa hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Kamanda Sirro amesema amepokea taarifa hizo kutoka kwa RPC wa Kinondoni kuwa amepokea taarifa hizo na vielelezo vipo.
“Oparesheni dhidi ya shisha bado inaendelea na leo RPC wa Kinondoni ameniambia wamekamata watu wa watatu na vielelezo kwahiyo vile vielelezo kwa kawaida vitapelekwa kwa mkemia wa serikali taratibu zitafanyika na watapelekwa mahakamani,”alisema Kamanda Sirro.
Aidha Kamanda Sirro amewaomba wananchi kupinga utumizi wa madawa hayo huku akiwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi.