Mtu
mmoja aliyejulikana kwa jina la Amina Hamisi (56) mkazi wa mtaa wa
mahina kata ya Butimba Jijini Mwanza, anashikiliwa na polisi baada ya
kumlazimisha mjukuu wake aliyejulikana kwa jina la Rehema Sadiki mwenye
umri wa miaka 7 kula kinyesi.
Kaimu
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Kamishina Msaidizi wa Polisi Augustino
Senga amedai kuwa tukio hilo limetokea Novemba 11, mwaka huu ambapo
mtoto huyo alikwenda chooni kujisaidia na kushindwa kumwagia maji ili
kuondoa kinyesi chake ndipo bibi yake ili kumuadhibu alimuamuru kula
kinyesi hicho kitendo ambacho mtoto huyo alikitekeleza.
Baada
ya tukio hilo kutokea raia wema walitoa taarifa polisi ambao walifika
eneo la tukio na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo.
Kamanda
Senga ametoa wito kwa wakazi wa jiii la Mwanza kutoa ushirikiano kwa
jeshi la polisi ili kudhibiti vitendo vya kikatili hasa kwa watoto
wadogo na kuongeza kuwa ukatili ni kosa kisheria hivyo wananchi waache
kufanya vitendo hivyo na watakao bainika sheria itachukua mkondo wake.