Hili linafanana na tukio la mkoani Mbeya ambapo mwanafunzi yule hakwenda hata nyumbani kwao kusema baada ya kupigwa na walimu kwa kuwa alikuwa ana kesi tatu nzito na aliwahi kumjibu hovyo baba yake mbele ya walimu alipokuwa ameenda kutetea asifukuzwe shule.
Achilia mbali hayo Mwanafunzi huyo alishawahi kuvunja TV ya baba yake nyumbani kwao kama wiki mbili zilizopita.
Pamoja na mambo yote hayo Wiki hili amekamatwa na walimu akiwa anavuta bangi shuleni na wenzake. baba yake mzazi hamtaki huyo Mwanafunzi lakini hana namna ya kumkabili.