Watoto wa Mboyelwa wameamua kugoma kuuchukua mwili wa baba yako kwa madai kuwa kifo chake kimesababishwa na uzembe wa wauguzi.
Mtoto wake, Bahati Chihula amesema Oktoba 6, mwaka huu alimfikisha baba yake katika hospitali hiyo kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji na kulazwa wodini.
Amesema juzi asubuhi wakiwa na baba yao wodini aliingia muuguzi na walinzi wanaolinda hospitali na kuwataka wanaowauguza watoke nje kwa kuwa muda wa kuona wagonjwa haujafika.
“Nilimuomba nesi (muuguzi) aniruhusu nimpeleke baba yangu chooni kwa kuwa alitaka kujisaidia, lakini nesi alikataa na kuniambia hiyo ni kazi yake, “amesema na kuongeza:
“Nilikubali kutoka na kumwacha baba yangu baada ya dakika chache nikiwa getini nilipigiwa simu kuwa baba yangu ameanguka chooni”.