Wimbo ‘Maria Salole’ wa Saidi Karoli ni miongoni mwa nyimbo za asili zilizofanya vizuri miaka ya 2000.
Hali hiyo iliufanya uongozi wa Diamond kuzungumza na uongozi wa Saida Karoli ili upate kibali cha kutumia sehemu za nyimbo hiyo.
“Tunakushukuru sana uongozi wa Saida Karoli na mzee Felician Mutakyawa kutupa haki na baraka zote kutumia wimbo wa Maria Salome,” aliandika Sallam instagram. “Tunatambua kwamba nyimbo hii itaendelea kuwa moja ya nyimbo bora kuwahi kutoka katika nchi ya Tanzania,”
Diamond kupitia wimbo huu amerudi tena katika nyimbo za asili baada ya kufanya vizuri na wimbo ‘Mdogo Mdogo’ miaka miwili iliyopita.