test

Jumamosi, 10 Septemba 2016

Wanakijiji walivyomcharaza bakora mwenyekiti wao!



 KAMA kuna kituko cha wiki ambacho kiliwagusa wananchi wengi ni habari za kucharazwa bakora na wananchi wake mwenyekiti wa kijiji kimoja katika wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya.
Kisa cha mwenyekiti huyo kucharazwa bakora ni kuwapelekea hesabu za mapato na matumizi ya kijiji yakionesha kwamba kijiji hicho kwa mwaka mzima kilikuwa na mapato kiduchu ya Sh 10,000 tu jambo ambalo liliwakasirisha wananchi hao.

Wananchi ni kama hawataki tena kudanganywa, huo wakati umeisha na sasa wanataka kuambiwa kitu halisi na sio kwenda kuwalisha matango pori.
Kitendo cha mwenyekiti kuwalisha matango pori wananchi wake ndicho ambacho kilisababisha wakasirike na kuamua kumcharaza bakora.
Unaambiwa siku ya mkutano, muitikio wa wananchi ulikuwa mkubwa na ndipo mwenyekiti alijitokeza mbele yao na kuanza kuwasalimia kwa mikogo na bashasha nyingi huku akichukua karatasi iliyokuwa inaonesha mapato ya Sh 10,000 ambazo pia zilitumika zote. Sh 10,000 kweli!
Hesabu hiyo ni wazi kuwa iliamsha hasira za wanavijiji ambao hawakukubaliana naye. Lakini msisitizo wa mwenyekiti huyo ulibaki palepale kwamba kwa mwaka mzima kijiji chao kimekusanya Sh 10,000.
Kilichowauma zaidi ni kwamba licha ya kusomewa mapato hayo kiduchu, lakini mwenyekiti huyo akawatia hasira zaidi kwa kuwataka waendelee kuchangia maendeleo ya kijiji chao ili kuepuka aibu hiyo ya kuingiza Sh 10,000 tu kwa mwaka.
Kwa habari zilizoandikwa kwenye midia ni kwamba hapo ndipo wanakijiji cha Rungwe walipoamua kumtia adabu mwenyekiti huyo 'fisadi' ili liwe fundisho kwa viongozi wengine wenye tabia hiyo. Kufumba na kufumbua wananchi wakawatuma vijana watatu kwenda porini kwenda kukata fimbo.
Mbele ya mke wake na watoto wake, mwenyekiti huyo alilala na akacharazwa fimbo na vijana walioshiba ambao walitumia fursa hiyo kumpa adhabu ambayo itafanya siku nyingine asiwe tena na hamu ya kupeleka hesabu ya uongo mbele ya wananchi wake.
Hatua hii ya wananchi kuamua kumcharaza mwenyekiti viboko ni uamuzi mgeni kabisa kwenye jamii yetu. Licha ya kuwa sio utaratibu mgeni kutumika maana huko nyuma tuliwahi kusikia mkuu wa wilaya akiwacharaza walimu viboko mbele ya wanafunzi wake kwa tuhuma za utoro.
Hivyo adhabu hizi za viboko kwa viongozi watu nadhani ni nzuri sana na sasa vijiji na majimbo pia yanatakiwa kuchukua mfumo huu kwa kuwacharaza fimbo viongozi wetu pale wanapokosea.
Kwa mfano mbunge kama akichaguliwa halafu akashindwa kuwapa maendeleo wananchi wake nao wamcharaze viboko! Kimsingi ni adhabu ya udhalilishaji lakini inaonesha kwamba wananchi hawataki kudanganywa, licha ya kuwa wengi wao hawakwenda shule, 

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx