Mh.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa dhati Kabisa kama Kijana
& Kada mtiifu wa Chama Cha Mapinduzi ninaetambua juhudi/Jitihada
zako unazozionyesha kila siku iitwapo leo za kuwaletea Maendeleo
Wananchi wako napenda kukupongeza kwa Kutimiza Ahadi yako ya kufufua
Shirika la Ndege la Taifa " ATCL" kwa kununua Ndege Mbili Mpya na leo
tumepokea Ndege ya Pili.
Sasa Watanzania Wote wamejionea wenyewe na Ulimwengu umejionea wenyewe ya Kwamba Tanzania Mpya yaja.
Mheshimiwa
Rais Hongera sana na Mungu akubariki, Akulinde na kukujaalia Afya njema
ili ukatimize vyema Majukumu yako ya kuwatumikia Watanzania kwa
Kuwaletea Maendeleo.
Robert PJN Kaseko
Mjumbe Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Arusha
September 27, 2016.