test

Jumamosi, 1 Oktoba 2016

Rais Magufuli Aahidi nchi kuwa na Jeshi Imara kuzidi majeshi yote duniani


Akizungumzia uimara wa jeshi hilo, Rais Magufuli alisema umetokana na misingi imara iliyowekwa na marais waliotangulia, huku akimshukuru Rais mstaafu Jakaya Kikwete kwa kuhakikisha ameliwezesha jeshi kuwa na vifaa imara, ambavyo jana vilitumika kuonesha uimara wa chombo hicho.

“Niwashukuru marais wote waliotangulia, ila nimshukuru sana Rais Kikwete yeye ndiye aliyewezesha jeshi kuwa na vifaa imara kama hivi, mimi sijanunua kitu hapa, siwezi kujisifu, ni juhudi za Kikwete na mimi nitaendeleza na kuhakikisha tunakuwa na jeshi imara na ikiwezekana kuzidi majeshi yote duniani,” alisema.
Akizungumzia ajira kwa JKT na mgambo, Rais alisema; “ Chief Secretary (Katibu Mkuu Kiongozi) kuanzia kesho (leo), hawa mgambo na JKT walioshiriki kwenye zoezi hili waingizwe kwenye ajira rasmi jeshini, nguvu zao hazipotei, hata kama hawajaenda mafunzo ya jeshi waingizwe wataenda baadaye.”
Katika hatua nyingine, alisema hafurahishwi na vitendo vya Jeshi la Magereza kuombaomba serikalini fedha kwa ajili ya kukarabati gereza mjini Bukoba lililoharibiwa na tetemeko na kuagiza ni marufuku fedha kutolewa kwa ajili ya ukarabati wake.
“Ni marufuku fedha kupewa Magereza kwa ajili ya wafungwa kwenye gereza lililoharibiwa na tetemeko, wale wanaotumikia adhabu wafanye kazi kujenga maeneo yaliyobomoka,” alisema.
Katika tukio hilo lililokuwa la aina yake, ndege vita saba zilipita kwa kasi angani huku zikidondosha mabomu, ambapo pia meli vita tatu zilijipanga baharini zikiwa na askari huku vifaru saba vikiwa baharini na kisha kwenda nchi kavu kumshambulia adui.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx